Jifunze Kitu Kwa Kila Mtu


Usiwachukulie poa watu ambao unakutana nao leo. Kila mtu ana funzo kubwa ambalo unaweza kulipata haijalishi mtu huyo amefanikiwa au hajafanikiwa. Bado kuna kitu kikubwa cha kujifunza kwake. 

Kama amefanikiwa hapo ndio unahitaji kujifunza mbinu alizotumia yeye mpaka kufanikiwa. Zitumie mbinu hizo kwa manufaa yako pia. 
Kama hajafanikiwa ila anapambana kuelekea ndoto yake, bado unaweza kujifunza kitu kwake. Unaweza kuona jinsi anavyo yachukulia maisha na hatua ambazo anachukua ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. 
Kama ni masikini na hana mwelekeo kitu kikubwa cha kujifunza kwake ni tabia ambazo zimemfanya awe alivyo kitu ambacho kitakusaidia wewe kuweza kuepukana na hizo tabia na hivyo kufanya kinyume chake. 
Kama alikuwa hawekezi, kwako utapaswa kuanzisha tabia ya kuwekeza. Kama alikuwa anatumia fedha hovyo basi wewe utapaswa kuanz kutumia fedha kwa mpangilio. Kama alikuwa na chanzo kimoja cha kipato, utapaswa kuongeza chanzo kingine cha kipato. 
Kwa vyovyote vile jifunze kitu kwa mtu yeyote yule unayekutana naye 
 KilaKheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X