Watu wengi wamekuwa wanapenda kuongelea fursa. ila wanasahau kuwa kitu kikubwa kuhusu #fursa siyo kuziongelea tu. badala yake kitu muhimu kuhusu fursa ni kuhakikisha kwamba unazichangamkia. hapa ndipo watu wengi wanafeli na hivyo kuendelea kupitwa na fursa zile zile ambazo wao wanaongelea kila siku kwenye vijiwe mitaani au kwenye mitandao ya kijamii. sasa ninachopenda wewe ufanye ni kuamua kuwa wa tofauti. badala ya wewe kuishia kuongelea fursa, basi chukua hatua na uzichangamkia hizo fursa.
kila la kheri