Kuna fedha naisubiri…


 

Imekuwa inatokea mara kwa mara watu wanaahidiwa fedha na kuanza kuweka mipango kamambe juu ya hiyo fedha. 

Hata hivyo huwa kuna mawili kwenye fedha ya kuahidiwa. Inaweza kutumwa kweli. Au isitumwe kabisa kitu ambacho kitakukwamisha au la utaendelea kusema, Kuna fedha naisubiri.

Unaweza kupanga kufanya mipango mingi kiasi kwamba fedha hiyo inapokuja, unashindwa kufanya maamuzi sahihi wa wapi pa kuielekeza hiyo fedha. Na hivyo kujikuta umetumia fedha  hovyo, huku mipango yako ikiwa haijatekelezwa.

Kwa hiyo kitu muhimu ninachotaka kukwambia ni kuwa usipigie hesabu fedha ambayo hauna. Usimwahidi mtu fedha ambayo wewe mwenyewe umeahidiwa.

Usihesehabu kuwa umeuza Kama hukappkea hiyo fedha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X