UKITAKA KUFANIKIWA UZA KWANZA VYOTE ULIVYONAVYO…


 

NB: Usiishie tu kusoma kichwa cha makala bila kusoma makala yenyewe

Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze vyote ULIVYONAVYO, kisha njoo unifuate -Biblia.

Kwenye Biblia kuna usemi huo wa kishujaa, ukieleza sifa moja muhimu ya kumfuata Yesu. Siku ya leo siyo kwamba ninataka nikuhubirie, hapana. Na wala siyo kwamba nitapenda ukauze ulivyonavyo ili Ufanikiwe, maana najua pengine wewe mafanikio unayotaka kupata ni mafanikio ya mali na fedha. Sasa hapo ukiuza ulivyonavyo itakuwaje?

Ninachotaka   kukwambia ni kuwa ukitaka kufanikiwa unapaswa kuachana na vitu vyote ambavyo vinakuzuia kuyafikia mafanikio, kisha kuiendea ndoto yako na malengo yako.
Vitu vyote na tabia ambazo siyo za muhimu kwa mafanikio yako unapaswa kuachana navyo ili uweze kuiendea ndoto yako kiroho Safi.

Sasa kazi ni kwako kujua ni vitu gani ambavyo unafanya japo siyo muhimu kwa mafanikio yako. Pengine ni ulevi wa pombe, mitandao, sigara au hata bangi. Pengine kuna vitu vinapoteza fedha zako kama kuhonga, kutumia fedha hovyo bila mpangilio au hata kucheza kamari.

Hivi ni vitu ambavyo utapaswa kuachana navyo kisha kuamua kuwekeza nguvu, muda, akili na kila kitu kwenye malengo na ndoto zako.

Ikumbukwe kuwa nguvu yako ya KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA haipaswi kugawanywa kwenye vitu vingi vingi ambavyo havina maana.
Unapojitoa kwa ajili ya mafanikio makubwa unapaswa kujitoa mzima, mzima. Hakuna kutafuta mafanikio nusu nusu (mguu mmoja unatafuta mafanikio na mwingine unafanya vitu vinavyokutoa kwenye mafanikio makubwa).

SOMA ZAIDI: FANYA KAZI KWA BIDII

Rafiki yangu, kwa Leo naishia hapo. Umekuwa nami.
Godius Rweyongeza

hakikisha umesubscribe kwenye channel yangu ya youtube kwa kubonyeza kwenye HAPA au video hii hapa chini


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X