Kitu kimoja kikubwa kuhusu wanaotimiza malengo siyo kwamba wana akili sana, au kwamba wamebarikiwa na Mungu kuliko wewe. Hapana. ila kitu ambacho kinawatofautisha na kitaendelea kuwatofautisha kwa siku nyingi ni kwamba.
1. wanaweka lengo wanalifanyia kazi mpaka linatimia. wanafanya hivi bila kujali wanapitia katika hali gani. bila kujali wamekutana na vikwazo gani. wao wanachojua ni kwamba msukumo wa kufikia lengo lao ni mkubwa kuliko kushindwa.
2. Wanaamua kujifunza kwa kina kuhusu lengo lao. wanajifunza mbinu, kanuni na vitu ambavyo vinawasaidia kuweza kufikia lengo lao.
3. Wapo tayari kuchukua hatua. hawaweki lengo na kutulia, ila hatua wanazochukua zinawatofautisha.
ANGALIA SOMO HILI: Usiishie tu kusema ONE DAY YES
4. wanatafuta konekisheni hata kama hawana. na kwenye zama hizi tunazoishi sisi kutengeneza konekisheni ni jambo rahisi sana. mtandao wa intaneti umekuja na maajabu yake. unakuwekeza mpaka kutengeneza konekisheni na mtu aliye ikulu hata kama wewe uko kijijini.
5. wanaweka siku ya mwisho (deadline) ya kufikia lengo lao, na hivyo kupata msukumo wa kulifikia lengo hilo kulinganisha na mtu ambaye hajaweka siku ya mwisho ya kufikia lengo.
6. Hawasubiri mpaka wawe na mtaji wa kutosha ili waanze. wanaanza na kisha kufanyia kazi kila kitu kinachokuja mbele yao