Wiki hii kwa ufupi: Masomo Sita Yaliyotikisa Wiki Hii


 

Juma la saba la mwaka 2021 limeshafika ukingoni. Ule mwaka uliokuwa unaonekana mpya sasa umeshaanza kuota mvi za uzee. Sio mpya tena.

Wengi walioweka malengo  wameshayasahau na wengine hawajachukua hata hatua moja kufanya kitu KUELEKEA hayo malengo yao.

Hili siyo mimi tu ninayelisema, bali tafiti za kitaalamu pia zinaonesha hivyo.

Tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya watu huwa wamesahau  malengo yao kufikia siku ya VALENTINE . Na unajua nini? Leo ndiyo siku ya valentine. Kheri ya siku hii ya kipekee kwako.

Lakini je, bado unafanyia kazi malengo yako ya mwaka huu? Umeshachukua hata hatua au unasubiri tarehe 31 Disemba ili lengo lako litimie kimiujiza. Kwa kulifahamu hilo, wiki hii nimekuandalia masomo makubwa sita ambayo nina hakika yatakuwa msaada kwako. Kazi yako ni kuchagua somo moja Kati ya haya sita kulifuatilia mwanzo mpaka mwisho, kisha uchukue hatua.

Mwisho kabisa, hakikisha umesubscribe kwenye channel yangu ya YouTube na ni ruksa kwako kusambaza masomo haya👇👇
Nakutakia kila la kheri.

1. Vitu Vitano Ambavyo Hupaswi Kuchoka Kufanya Mwaka Huu

https://youtu.be/W3-BvtI79wk

2. Kitu Kimoja Muhimu Kuhusu Fursa (dakika 1:30)

https://youtu.be/gFrrjGYMWn4

3. Vitu Vitano Vya Kutahamu Kuhusu Fursa
https://youtu.be/XDTncF6Tyms

4. Vitu Vitano Vinavyofanya Vijana Wengi Kufeli Haraka Sana
https://youtu.be/kbGVBrurfxc

5. Friday Motivation Video: Usiishie tu kusema one day yes.

https://youtu.be/DbSt-x6uHcg

6.  Vikwazo VitanoVinavyokuzuia Wewe Kufikia Malengo Yako 2021 
https://youtu.be/p9I8jxMJiYw

Hayo ndiyo masomo tuliyopata ndani ya juma hili hapa. Je, ni somo gani limekuwa msaada mkubwa kwako?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X