Kitu muhimu kitakachokutofautisha wewe na watu wa kawaida


 

Kuna vitu ambavyo watu waliofanikiwa na watu waliobobea huwa wanafanya ila watu wa kawaida huwa hawavifanyi. Mojawapo ya kitu hicho ni kufanya kazi kila siku bila kujali kitu gani ambacho kinatokea. Ujue kila mtu anaweza kufanya kitu chochotge kwa kujiskikia kisha akaacha, ila watu waliofanikiwa hawafanyi vitu kwa kujisikia au kutojisikia. Bali wanafanya kwa sababu kitu hicho wameamua kukifanya kwenye maisha yao,

Kila mtu anaweza kuwa mtu wa kuweka akiba kwa kujisikia. Kila mtu anaweza kuandika pale anapojisikia. Kila mtu anaweza kufanyia kazi kipaji chake anapojisikia. Ila watu waliofanikiwa wamejiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanafanya hicho kitu bila kujali wanapitia kwenye mazingira gani, Wanafanya mazoezi hata kama siku hiyo hawajisikii kufanya hivyo, hivyo basi na wewe unapaswa kuwa mtu wa aina hii.

Na kitu hiki hapa nakuhakikishia kuwa kinaenda kukutofautisha wewe na watu wengine wote. Hii ni kutokana na ukweli kuwa hutakuwa tu ni mtu wa kufanya kazi kwa kujisikia bali utakuwa ni mtu wa kufanya kazi bila kujali unapitia katika hali gani na hivyo kujenga upekee wako

 

Hakikisha umesoma makala hii hapa: JITUME KWA FAIDA YAKO

 

Pia angalia video hii hapa

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X