Njia rahisi ya wewe kupoteza fedha ni pale unapoanza kutumia fedha yako ili kuwaonesha watu kuwa una fedha. Pale unaponunua vitu ili watu wajue kuwa una fedha.
Hapo unakuwa umeingia kwenye mtengo mbaya ambao unakufanya usiishi maisha yako, badala yake unaanza kuishi maisha kwa kuangalia wengine watakuonaje. Ni mtego mbaya maana mwisho wa siku utajikuta unanunua vitu ambavyo wewe mwenyewe huvihitaji. Na kwa maneno ya Warren Buffet, ukinunua vitu ambavyo huvihitaji itafikia hatua ambapo utauza mpaka vitu unavyovihitaji ili kupata fedha.
Kazi muhimu ya kufanya siku ya leo. Usinunue au kufanya vitu ili kuwaonesha watu kuwa una fedha. Kila la kheri.
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza