Imepita 9 hivi tangu niliposoma riwaya ya S. N. Ndunguru inayoitwa The Divine Providence.
Kiufupi ukiniambia nikuueleze riwaya hiyo hata kwa ufupi, siwezi kusema chochote kuhusu hiyo riwaya. Sikumbuki hata ilikuwa inahusu nini.
Isipokuwa nakumbuka kitu kimoja tu kutoka kwenye ile riwaya. Kitu hiki sijawahi kukisahau na wala sitakuja kukisahau. Na kitu hiki kinakutwa kwenye sura moja ninayokumbuka iliitwa THE EVIL WILL OUT.
Kwenye sura hii nilijifunza kuwa; ukifanya uovu kwa kujificha, jua kuwa siku moja huo uovu unaenda kujulikana. Hakuna kitu ambacho utafanya kwa kificho kikaendelea kuwa kificho maisha yote. Ipo siku tu huo uficho wako utagundulika.
Kwa hiyo kinyume chake, ni kuwa unapaswa kuwa mtu wa haki, kusimamia ukweli na kuuishi.
Nenda sasa kwenye YouTube Channel yangu na ufuatilie somo hili hapa