Kama unataka kuwa na maisha bora na yenye maana, anza kwa kuwa na lengo ambalo unaenda kufanyia kazi maishani mwako.
Kuwa na lengo tu kunaweza kukufanya ubadili tabia zako na mambo mengine yote.
Kutakufanya upangilie ratiba zako upya.
Kutakufanya ubadili namna ya unavyonunua vitu na kutumia fedha zako n.k.
Kitu hiki kitalaamu kinaitwa Diderot effect. Diderot ni jina la mtu. Miaka mingi iliyopita mtu huyu ambaye jina lake kamili ni Denis Diderot alikuwa mwanamashairi mzuri sana, ila hakuwa na fedha. Sasa ilifika wakati ambapo alitakiwa kufanya harusi ya bintiye.
Habari za kuwa hakuwa na fedha ya harusi zilisambaa, mpaka zikamfikia mwana wa mfalme aliyekuwa anazikubali kazi zake za ushairi.
Mwanamfalme akaamua kununua kazi zake kwa bei kubwa sana.
Ghafla, Diderot akawa tajiri ndani ya siku moja. Akawa na fedha ya sherehe na ziada. Ndipo alipoamua kununua nguo. Kutokana na uzuri wa nguo ile, ilionekana nguo hiyo haiendani na eneo alipokuwa anakaa. Hivyo, aliamua kubadili mwonekano wa ndani ya nyumba yake. Alivyobadili mwonekano wa ndani akagundua kuwa vitu vingine ndani pia haviendani na huo mwonekano mpya na vyenyewe vilipaswa kubadilishwa. Muda siyo mrefu alikuwa anabadili kila kitu kitu kilichompelekea kurudi kwenye umasikini na madeni makubwa.
Sasa hiki kitu siyo tu kuwa kilitokea kwa Diderot pekee bali huwatokea watu wengi. Mtu ananunua kitu kimoja mwisho wa siku anajikuta amenunua mpaka vitu vingine ili viendane na hicho kitu. Na hicho kitu kwa sasa kinajulikana kama DiderotEffect.
Ila unaweza kukitumia kwa namna chanya, kwa kuanza kufanyia lengo lako moja, likakupelekea kwenye lengo jingine.
Tuseme labda una lengo la kusafiri nje ya nchi. Lengo hili linaweza kukupelekea wewe kuanza kuweka akiba, kufanya mazoezi, kula vizuri, kiwekeza, kutumia mtandao wa intaneti kwa namna chanya n.k.
Hiyo ndiyo nguvu ya lengo moja, hakikisha unaanza kuitumia kuanzia leo.
*MUHIMU SANA*
Kabla mwezi huu haujaisha hakikisha umejipatia nakala yako ya KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa bei ya punguzo babu kubwa. Utalipia 7999 tu badala ya 10,000/-. Mwisho wa ofa ni tarehe 31 mwezi huu. Kitabu kinapatikana kwa mfumo wa nakala ngumu (hard copy).
Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili upate nakala yako.
Kumbuka, *kesho yako ipo mikononi mwako.* Chukua nakala hii nawe utaona kwa nini 2021, haitakuwa sawa na 2021 uliyokuwa nayo kichwani mwako.
2 responses to “Nguvu ya lengo moja kuelekea mafanikio makubwa”
[…] Nguvu ya lengo moja kuelekea mafanikio makubwa […]
Undeniably imagine that which you stated. Your favourite justification seemed to be on the net the easiest thing
to be mindful of. I say to you, I definitely get irked at the same time as people think
about issues that they just don’t recognise about.
You managed to hit the nail upon the top as neatly as outlined
out the entire thing without having side effect , other folks can take a signal.
Will probably be back to get more. Thanks