Mara nyingi huwa tunatafuta ubaya au kitu kibaya kinachoonekana kwa wengine. Ndiyo maana wengi wanapenda umbea kwa sababu unakutanisha watu ili kuwasema wengine.
Kitu kimoja kikubwa tunachojifunza leo ni kuwa mbali na mapungufu ya watu, mabali na makosa yao. Bado kuna vitu ambavyo wanaweza kufanya vizuri. Kuna vitu vizuri kutoka kwa kwa hao watu ambavyo ukiangalia vizuri utaviona. Pengine vitu hivi siyo kumi au vitano. Ila hata kitu kimoja tu kinatosha kabisa.
Ebu kuanzia leo anza kuangalia uzuri kwa wale unaokutana nao. Wanaweza kuwa rafiki, ndugu, wafanyakazi wenzako/wako, mwenza wako n.k. ni kitu gani kimoja kizuri unakiona kwao?
Ni kipi?
Kione hicho na weka nguvu zako kwenye uzuri wake. Kitu hiki kinaweza kuwa ni tabasamu la mtu huyo, urembo/utanashati, chakula kizuri, kazi nzuri n.k.
Kiufupi, tafuta kitu kizuri ambacho unaweza kumsifia mtu leo na ufanye hivyo.
Kila la kheri