Ujumbe Muhimu Watu Ambao Wanahitaji Kutoka Kwako


 

Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Kuna kitu kimoja ambacho watu wanahitaji kutoka kwako rafiki yangu. Na kitu hiki hapa ni ujumbe wa matumaini. Watu wanahitaji sana ujumbe wa matumaini kutoka kwako. Ujue tunaishi kwenye ulimwengu ambapo watu wanakatishwa tamaa sana, taarifa za habari nyingi zinaoneshwa katika namna ya kukatisha watu tamaa. Utasikia kuwa sehemu fulani kuna mapigano, basi hicho kitu kidogo tu kinaoneshwa na kuzunguzwa kwenye mitandao kwa nguvu zote wakati sehemu zenye amani zikiwa ni nyingi lakini zikiwa hazisambazwi.

 

Ikitokea dereva akasababisha ajali, basi siku hiyo hiyo ajali inaongelewa sana kama vile hakuna madereva wengine waliofikisha watu salama. Wakati uhalisia unakuwa ni kwamba dereva mmoja kasababisha ajali ila kuna maelfu ya madereva waliondesha magari vizuri na kufikisha abiria wao salama.

 

Kumbe kwa hali hii ni wazi kuwa watu wanahitaji ujumbe mkubwa wa matumiani kutoka kwako kuliko ambavyo wanahitaji kitu kingine chochote. Watu wanahitaji wewe uwape moyo ili waone kwamba na wao wanaweza kufanya makubwa, waone kwamba na wao wanaweza kuwa watu wa maaana kwenye hii dunia. Watu wanahitaji ujumbe wa matumaini ili na wao waweze kufanikisha ndoto zao badala tu ya kuishia kukata tamaa. N

 

Kuna utafiti ambao ulifanyika ukaonesha kuwa mtu wa kawaida kwenye maisha yake walau anakutana na watu wasiopungua elfu kumi. Hii ndiyo kusema kwamba kama wewe ni mtu wa kawaida, mpaka unafikia siku ya kufa utakuwa umekutana na watu siyo chini ya elfu kumi. Hawa ni watu ambao unaweza kufanya kitu kwao, kuongeza kitu au hata kuwainua. Ila ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, huhitaji kuwapa matumaini watu wote hao. Wewe anza na watu kumi tu, inatosha. Ukiweza kuwapa matumaini watu 10, nao hao watu kumi wakaenda wakawapa matumiani watu wengiine kumi. Ndani ya muda kidogo utakuwa umeweza kuibadili dunia.

Rafiki yangu, huo ndio ujumbe wangu mfupi kwako siku ya leo. Nina hakika kwamba unaenda kuufanyia kazi ujumbe huu.

Tukutane kwenye jukwaa la wanamfanikio.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X