USIFANYE UWEKEZAJI WOWOTE ULE BILA KUJUA KITU HIKI


 

Kama una mpango wa kuanza uwekezaji sehemu yoyote ile, hakikisha kwamba hauanzi kufanya uwekezaji bila kuwa na elimu na maarifa ya kutosha kuhusu uwekezaji ambao umeamua kuufanya.

Ni bora uendelee kukaa na fedha zako kwa kipindi hiki ambacho hauna maarifa kuliko kuzitoa sadaka na kuwekeza bila ya maarifa sahihi kwenye kile unachoweza.

Au la ni bora utumie kiasi Cha FEDHA kutafuta maarifa sahihi kwanza ili uweze kuwekeza ukiwa umejiimarisha kimaarifa.

Kitendo cha kuwekeza bila uelewa wa kutosha kinaweza kukupa hasara kubwa na pengine kukufanya upoteze fedha zako zote.

Unawexa kujiona mjanja na kuamua kukwepa gharama za kutafuta maarifa sahihi, ila ukajikuta kuwa umepoteza fedha zaidi ya kile kiasi ambacho ungetumia kwenye kutafuta maarifa.

Kitu hiki kinaweza kukupelekea wewe kuanza kutafuta maarifa na elimu sahihi ya uwekezaji baada ya kuwa umepoteza kwenye uwekezaji wa kwanza.

Kitu muhimu hapa unachopaswa kuondoka nacho siku ya leo ni kuwa. Usianze uwekezaji bila ya kuhakikisha umetafuta maarifa sahihi.
Na baada ya kuanza uwekezaji, usiache kutafuta maarifa sahihi. Endelea kutafuta maarifa sahihi siku zote na Mara zote.

Kila la kheri

Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X