Marafiki ni watu wa muhimu Sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Wanatusaudia kufanya mambo mengi Sana. Imegundulika pia kuwa marafiki wazuri ni chanzo cha furaha miongoni mwa watu. Huku marafiki wabaya wakiwa ni chanzo cha huzuni na karaha. Siyo Hilo tu marafiki wazuri wanaweza kukufanya usonge mbele na kufanikisha malengo yako au la urudi nyuma na hivyo kushindwa. Jim Rohn aliwahi kunukuluwa akisema kuwa wewe ni matokeo ya watu watano waliokuzunguka. Hii ndio kusema kwamba kama umezungukwa na vilaza watano, basi wewe utakuwa ni kilaza wa sita. Kama umezungukwa na wawezekazi watano basi wewe utakuwa mwekezaji wa sita. Hivyo hivyo, kama umezungukwa na wachapakazi watano basi wewe unakuwa mchapakazi wa sita. Hivyo, ni muhimu sana tufahamu sanaa ya kutengeneza marafiki wazuri. Maana kipato chako, elimu, uelewa na hata maamuzi unayoyafanya yanaathiriwa sana na wale watu waliokuzunguka.
1. Kama unataka marafiki wazuri, anza wewe kuwa mzuri. Huu ni ujumbe kuntu Sana ambao unapaswa kuufahamu mara moja. Huwezi kuwa unahitaji marafiki wazuri wakati wewe mwenyewe unaendelea kufanya mambo ya hovyohovyo na yasiyoeleweka. Anza kuwa mzuri, marafiki wazuri watakuja.
5. KAMA HUJAPATA MARAFIKI WAZURI BASI VITABU VINAWEZA kuwa Marafiki Wazuri kwako. Hivyo basi tumia muda mwingi ukiwa unasoma vitabu. Kusoma vitabu kunakukutanisha na watu wengi hata Kama wapo mbali.
Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri