SABABU 2 kwa Nini kila ukipata fedha unasahau mipango yako yote


 

Kuna watu wengi ambao wasipokuwa na fedha wanakuwa na mipango lukuki, ila siku wakipara hiyo fedha, mipango yao inayeyuka kwanza, halafu ndipo wanakuja kuikumbuka baadaye sana baada ya kuwa wametumia fedha zikaisha.

Sasa zifuatazo happy chini ni sababu 2 za kwa nini kila ukipara fedha mipango yako inateyuka kwanza

1. Hauna malengo madhubuti
Kinachokupelekea wewe kutumia fedha zako mpaka zikaisha ni kwa sababu mipango yako au malengo yako siyo madhubuti.
Moja, hujaandika chini malengo yako kitu kinachopelekea wewe kufanyia kazi mpango wowote unaokuja kwako Mara tu baada ya kuwa umeshika fedha.

2. Bado unatawaliwa na hisia za fedha kwenye maamuzi yako.
Watu wengi wakishika fedha ni Kama vile huwa wanapoteza akili yao ya asili na hivyo kutawaliwa na hisia kwenye maamuzi. Kitu muhimu cha kufahamu hapa ni kuwa kila unaposhika fedha unapaswa kuiacha fedha hiyo itulie kwa kipindi cha wiki moja na zaidi kabla hujaitoa na kuanza kuitumia.

Endapo wazo la kununua kitu fulani litakujia ndani ya hiki kipindi. Basi kiandike hicho kitu pembeni, kisha usubiri baada ya wiki uone Kaka bado utakuwa unakihitaji. Kwa njia hi utajiepusha Sana kununua vitu visivyokuwa vya lazima na hivyo kuweka nguvu zako kwenye mipango yako.

Soma Zaidi: Ijali Sana Fedha Yako

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X