Huduma Sita Muhimu Unazoweza Kupata Kutoka Kwangu


Habari yako rafiki yangu. Siku ya leo nimeona nikushrikishe huduma  ambazo unaweza kupata kutoka kwangu.

1. HUDUMA YA VITABU
Mpaka sasa nimeandika vitabu 16. Unaweza kuona baadhi ya vitabu hivyo hapa. Chagua kitabu chochote unachoona kinakufaa, Kisha jipatie nakala ya kitabu husika. BONYEZA HAPA KUONA ORODHA YA VITABU VYANGU VYOTE.

2. HUDUMA YA KUJIFUNZA UANDISHI
Moja ya ujuzi muhimu unaopaswa kuwa nao maishani ni ujuzi wa kuandika. Jifunze uandishi hata Kama hujawahi kuandika sentensi moja, maishani mwako. Huduma hii inakufaa sana wewe maana ni wazi kuwa katika maisha Kuna wakati utapaswa kuandika, iwe ni kuandika kitabu, makala, pendekezo, andiko la kushawishi watu, ushauri n.k. Sasa kwa nini usijifinze kwa kina kuhusu uandishi na kuujua nje ndani. Ndio maana ninekuandalia kozi hii muhimu sana ya uandishi. Kwa elfu 70 tu, unaweza kujifunza uandishi na kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi kutoka kwangu. Kozi hii hudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kama una mpango wa kuandika kitabu, kozi hii pia inakuhusu. Jiunge ili uweze kujua mengi juu ya uandishi wa vitabu.

3. JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWA KUTUMIA BLOGU
Kuna kipindi nilikuwa nasikia kuwa akina Millard Ayo wanatengeneza fedha kupitia mtandao wa intaneti. Swali langu likikuwa wanawezaje? Wanaanzia wapi, na je hili linawezekana kwangu? Baada ya kufuatilia kwa kina hatimaye, ndipo nikikuja kugundua kuwa kumbe hata Mimi naweza kutengeneza fedha mtandaoni. Na sehemu ya kuanzia kabisa ni kwenye blogu. Tangu nimeanzisha blogu yangu, sijawahi kujutia maana imekuwa chanzo Cha kipato, kisichokauka. nilianza kutengeneza fedha kupitia blogu mwaka 2017 na tokea hapo nimeendelea mpaka leo.

Ningependa kukuonesha na wewe jinsi ya kutengeneza fedha kwa kutumia blogu. Nitakufundisha na kukuonesha kila kitu unachohitaji kujua KUHUSU BLOGU na jinsi ya kutengeneza fedha fedha.
Unaweza kuanzisha blogu hata Kama uko bize. Kuna namna nzuri ya kuiendesha ambayo ukiijua itakusaidia sana.
Blogu ni kama ATM ya benki. Inafanya kazi saa 24 hata kama umelala, umesafiri au upo likizo. Blogu yenyewe hajali, haidai mapumziko wala likizo na wala hata haiitishi mgomo.
Kupata kozi hii utalipia elfu 70 na kozi hii itadumu kwa mwezi mmoja tu. Baada ya hapo utakuwa umeiva kwa asilimia 100. Kama utahitaji usimamizi zaidi baada ya hapo utalipia elfu 20 kila mwezi.

N.B. 1. UKITAKA KUPATA KOZI YA UANDISHI pamoja na KUTENGENEZA FEDHA KWA NJIA YA BLOGU kwa pamoja, utalipia laki moja (100,000)/- badala ya laki moja na elfu arobaini (140,000).

2. Kama umekosa ajira na ungependa kuanza kujikwamua, hizi kozi mbili hizi zinaenda kuwa daraja kubwa sana la kusonga mbele.

4. GHOST WRITING
Hii ni huduma ambayo ninakusaidia wewe kuandika kitabu, kisha kukikabidhi kwako na mwandishi anakuwa ni wewe.

Kwa huduma hii unaweza kuwa na wazo ambalo mimi nitakusaidia kusaidia kulikuza na kuliweka vizuri kwenye mfumo wa kitabu.

Kama hauna wazo tutaongea na nitakusaidia pia.

Kama una kila kitu cha kuandika ila bado uko bize na hauna muda wa kutosha wa kuandika, basi pia wewe hii huduna unaihitaji.

Gharama za ghost writing hutegemea na kitabu husika na
Uharaka uliopo kuanzia kazi inapoanza mpaka kukamilika.
Hivyo wasiliana nami kwa 0755848391 tuongee nikusaidie wewe kuandika kitabu chako.

5. HUDUMA YA UKOCHA
Hii huduma ambapo Mimi ninakuwa nyuma yako kwenye kazi au kitu ambacho unafanya. Ninakufuatilia kwa ukaribu wewe ukiwa mtendaji mkuu na Mimi nikiwa msimamizi wako kuhakikisha unafanikisha hicho kitu.
Nitaweza kukusimamia katika biashara zako.
Usomaji wa vitabu
Usimamizi wa fedha
Afya na mahusiano
Kipaji chako
Uneni (public speaking)
Au kitu kingine tutakachopanga

6. CONSULTANCY na LIVE PERFORMANCE
Hapa ni pale utakapokuwa unahitaji kukutana nami ana kwa ana ana (consultancy) au unahitaji nije kutoa  kufundisha kwenye semina.

Gharama za consultancy ni laki moja kwa saa. Na gharama za mimi kuja kwenye semina siyo chini ya laki saba.

Kama kuna  huduma yoyote kati  ya hizo  hapo juu, basi, wasiliana nami kwa 0755848391 ili uweze kuipata


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X