Jiandae kufanikiwa


 

Mafanikio hayatakuja kwako Kama ambavyo jua linawaka kwa kila mtu, badala yake wewe unapaswa kujiandaa kwa ajili ya kufanikiwa. Tengeneza mazingira yanayovuta mafanikio kuja kwako.
1. Anza kuishi tabia za kitajiri kama kuweka kuweka akiba, kuamka mapema, kufanya tahajudi (meditation), kuweka malengo na Kuyafanyia kazi

2. Fanya kazi kwa bidii maana mafanikio halisi hayaji kwako ukiwa umelala.

3  Anza kujisemea maneno chanya. Kumbuka maneno huumba.

4. Penda mafanikio ya watu wengine na kamwe usije ukawavuta wengine chini ili waanguke na wewe uinuke.

5. Fahamu kuwa mafanikio yako yanategemea na jinsi ambavyo wewe unahusiana na watu. Maana vitu vingi unavyogitaji (fedha, ujuzi, konekisheni n.k) wanavyo watu.

Rafiki yangu hivyo hapo ndivyo vitu unaweza kuanza kujiandaa kufanikiwa. Kumbuka kwamba mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa nayo. ila tofauti na haki nyingine ambazo unaweza kwenda mahakamani kuzidai, mafanikio yako hayadaiwi mahakamani. Badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuyapigania kwa kufuata kanuni za mafanikio. Kila la kheri.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X