Kutana na Zhang Yiming, Billionea wa Kichina Na Mwanzilishi Wa TikTok Pamoja Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake


 

Zhang Yiming ni mwanzilishi wa mtandao wa kampuni mama ya ByteDance ambayo ipo nyuma ya mtandao Tiktok. Billionea huyu aliyezaliwa mwaka 1983 ana utajiri wa Zaidi ya bilioni 44. Siku siyo nyingi bilionea huyu alistaafu uongozi wake kwenye kampuni yake huku akisema kuwa kwa sasa anaenda kujisomea vitabu ili aweze kupata mawazo mengine mazuri zaidi.

Unaweza kusoma ujumbe huu mfupi ulioandikwa na SwahiliTimes.

Kustaafu kazi ajili ya kusoma vitabu kunaweza kuwa Ni kitu cha kushangaza hasa katika jamii yetu ya kiafrika ambapo usomaji wa vitabu ni janga kubwa na watu wengi hawapendi kusoma vitabu hata wale wanaojiita wasomi. Wakati wasomi wetu wanahangaika na vyeti mtaani na wanajidai kuwa hawawezi kusoma vitabu maana walishahitimu chuo, jamaa anaacha kazi ili kusoma vitabu. Sasa yafuatayo ni mambo matano ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa.

Kwanza, ni utaratibu wa kujisomea vitabu. Huu ni utaratibu ambao unapaswa kuwa nao. Soma vitabu kadiri uwezavyo maana vitabu vina maarifa mengi sana ambayo yatakusaidia wewe kuweza kuendelea kusonga mbele. Kwenye vitabu unaweza kupata mawazo mapya ya kufanyia kazi, msukumo mpya na hata njia mpya za kuyaendea maisha na hivyo kukufanya wewe uzidi kuboresha maisha yako. Hii haimaanishi kuwa na wewe uache kazi ili usome vitabu, au usiendelee kutafuta kazi kwa kisingizio Cha kusoma vitabu. Hapana. Soma vitabu ukiwa hapo hapo ulipo sasa.

Pili, Tunapaswa kujitafuta na kujijua zaidi kila mara. Pale unapohisi kama Kuna kitu cha zaidi ambacho unahitaji maishani mwako ila hujui namna ya kukipata, basi unaweza kusoma vitabu.

Tatu,aa Unapofanya kitu na kulikamilisha, usiridhike na kuishia hapo. Angalia wapi unaweza kufanya kazi zaidi na kufanikisha kingine. Safari yako moja iwe chanzo Cha kuanzisha nyingine.

Nne, Hakuna kulala hata kama una utajiri mkubwa. Endelea kufanya kitu na kuja na mawazo yatakayosaidia watu zaidi.
Kwa utajiri alionao huyu jamaa angeweza kulala na kula tu. Ila bado anasema anaenda kutafuta mawazo mengine ya kufanyia kazi. Hii ndiyo kusema kwamba tunapaswa kuutumia vizuri muda wetu wa kuwa hapa duniani maana baada ya kifo Kuna siju nyingi za kulala makaburini.

Tano, kwenye maisha unapaswa kufanya uamuzi na kuusimamia uamuzi wako. Maana hata usipofanya uamuzi Kuna watu watakusaidia kuufanya huo uamuzi.

Soma zaidi: Ushauri Wa Mhe. JakayaMrisho Kikwete Kwa Kijana Anayetaka Kufanikiwa

Kila la kheri.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X