Maeneo Matano Yanayopoteza Fedha Zako Na Jinsi Unavyoweza Kuipata Fedha Hii Kwa Ajili Ya Akiba


Kuna vitu ambavyo unafanya au kununua na vitu hivyo vinakupelekea wewe kupoteza fedha ambayo ingekuwa msaada kwako. Sasa siku ya leo ningependa kukueleza vitu vitano vinavyokufanya wewe upoteze fedha. Fedha hii inaweza kuwa kianzio kwako kwenye masuala mazima ya kuweka akiba.

MOJA, KUNUNUA au KULIPIA VITU UNAVYOWEZA KUFANYA
Kuna vitu ambavyo wewe mwenyewe unaweza kufanya kwa muda na vikawa msaada na muda mwingine kukusaidia wewe usipoteze fedha zako hovyo. Mfano, unaweza kujifunza vitu kidogo kuhusu kifaa chako cha moto, hivyo kuepuka kwenda kaa fundi kila mara, hata kwa jambo dogo sana. Au unaweza kujifunza kutengeneza vitafunwa na hivyo kuepuka kununua vitafunwa kila mara.

PILI, KUFANYA MANUNUZI MADOGO MADOGO ILA MENGI
Kununua matumizi madogo madogo kunaweza kukufanya utumie gharama kubwa ukilingamisha na pale ambapo ungenunua matumizi yote kwa pamoja. Hivyo, jifunze kufanya matumizi yako kwa pamoja. Mfano, badala ya kununua kitunguu kimoja kila siku, unaweza kuamua kununua kilo ya vitunguu. Hii kwa muda mrefu ina faida kubwa ukilinganisha na ule ununuaji wa kitunguu kimoja.

3. KUFANYA MIAMALA MINGI MIDOGOMIDOGO.
Kama ilivyo kwa MANUNUZI MADOGO MADOGO, ndivyo ilivyo pia kwa MIAMALA MIDOGO MIDOGO. Hivyo ili kuepusha makato yasiyo ya lazima basi jitahidi kuwa unafanya MIAMALA kwa pamoja. Muda mwingine unaweza kwenda kwa wakala na kutoa fedha Kisha kuwatunia wengine ili kuepusha kukatwa kwa kila muamala utakaotuma.

4. KUJIUNGA VIFURUSHI MITANDAO MINGI KWA WAKATI MMOJA
Kabla hujajiunga na vifurushi mitandao tofauti tofauti jiulize Ni kweli unavihitaji?  Ni bora kujiunga na kifurushi cha mtandao mmoja utakaoutumia kuliko kuwa na vifurushi vya mitandao mingi usiyoitumia.

5. KUFANYA MATUMIZI YA BENKI KWENDA SIMU
MIAMALA ya kibenki kwenda mitandao ya simu ina makato makubwa. Na hata MIAMALA ya mtandao mmoja kwenda mwingine nayo hivyohivyo. Hivyo, wewe tafuta namna ya kuipunguza.

6. KUFANYA MIAMALA YA KIBENKI  KWA WAKALA
SIKU hizi maisha yamekuwa rahisi sana. BENKI zipo kiganjani, BENKI zipo mitaani. Uwepo wa mawakala BENKI husika wanasaidia kuweka na kutoa fedha haraka. Hata hivyo, utoaji wa fedha kwa wakala una makato makubwa ukilinganisha na pale unapotoa ATM.

Rafiki yangu, hiyo hapo ndiyo mianya mitano inayopoteza fedha zako, ukiiepuka utaweza kupata fedha za kuweka akiba. Kila la kheri.

SOMA ZAIDI: 

MAKOSA 50 AMBAYO WATU HUFANYA KUHUSU FEDHA: KOSA LA #3 KUDHARAU UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X