Mo Dewji Atoa Siri Tano Zilizomfanya kufanikiwa Sana


Siku ya leo nimeona nikusogezee siri tano za mafanikio kama ambavyo Mo Dewji amezitaja kwenye mojawapo ya Twitter yake.

Kwenye hiyo Twitter, Mo Dewji anasema;

Toka nikiwa kijana nilikuwa na ndoto ya kuwa mjasiriamali.
Safari ya ujasiriamali imejaa vikwazo matuta na kona nyingi. Unahitaji kuwa na nidhamu, ustahimilivu na zaidi adabu, kadri unavyosonga mbele
Kutumia njia za mkato hazitakusaidia kufahamu au kufikia malengo kistahiki.

Huo ndio ujumbe wa Mo Dewji ambao tukiuchambua kiundani tunakutana na vitu vitano kuhusu ndoto na mafanikio. Kiufupi Mo Dewji kwenye Twitter hii ameeleza vitu vingi vikubwa kuhusu mafanikio kwa wakati mmoja. Kwa hiyo ujumbe huu siyo tu kuangalia na kupita, bali tunapaswa kuutafakari kiundani kabisa na ndiyo maana hapa chini nimekuwekea vitu vitano kutoka kwenye huo ujumbe, huku nikidadavua kiundani.

Kwanza, unapaswa kuwa na ndoto kubwa sana.
Kama unavyoona Mo mwenyewe anasema ndoto yake ya kuwa mjasiriamali amekuwa nayo tangu akiwa kijana.  Inashangaza kukuta kwamba vijana wengi mtaani hata hawana ndoto ya maisha yao. Hawajui wapi wanataka kwenda wala nini wanahitaji kupata maishani mwao. Ukiwauliza una mpango gani miaka mitano au kumi ijayo, utashangaa kuona wanasema kwamba miaka kumi ni mingi sana. Hili ni jambo la kushangaza na kustaajabisha, maana mtu asipokuwa na ndoto kubwa maishani mwake hatakuwa na mwelekeo wala sehemu ya maana anapoelekea, yeye atakuwa ni mtu wa KUZUNGUKA huku na kule akifanya hiki na kile bila mwelekeo. Ila unapokuwa na NDOTO maana yake maisha yako, malengo yako, na rasilimali zako zote unazielekeza kwenye kufanyia kazi hiyo ndoto yako. Na hili siyo tu kwamba ni jambo la kubahatisha, bali mpaka vitabu vitakatifu vimeandikwa kuwa pasipokuwa na maono watu huangamia.

Soma zaidi; Nukuu Tano Zilizokonga Nyoyo Za Watu Kutoka Kwenye Kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

Pili, Safari ya ujasiriamali imejaa vikwazo matuta na kona nyingi
Haijawahi kuwa rahisi na wala haitakaa iwe rahisi kufikia ndoto yoyote unayojiwekea. Kuna vikwazo vingi hutokea kwenye safari. Kuna vikwazo kutoka ndani yako nwenyewe, vikwazo kutoka nje (watu waliokuzunguka, mazingira n.k) lakini kwa mtu mwenye ndoto vikwazo ni sehemu tu kusongambele. Haina kufeli. Kila unapokutana na kikwazo au changamoto unapaswa kuitatua na kusongambele ili ufanikishe ndoto yako.

Tatu, Unahitaji kuwa na nidhamu,
Nidhamu ndiyo kila kitu. Huwezi kufanikiwa bila ya kuwa na nidhamu. nidhamu ya fedha, nidhamu ya muda na nidhamu ya kila kitu unachofanya. Ndio maana muda mwingine watu waliofanikiwa huwa wanawasemwa kuwa  wametoa kafara. Unakuta mtu amejijengea nidhamu ya kufungua ofisi yake asubuhi na mapema sana (kabla watu wote hawajafungua) na kuifunga usiku sana (baada ya WENGINE wote kufunga). Sasa watu wakiona hivi wanasema huyu alitoa kafara na mganga akamwambia awe anafungua mapema na kuchelewa kufunga, kumbe ni nidhamu.

Unakuta mwingine hanunui hata nguo ili kupata fedha ya kuweka akiba, ila watu wakiona wanasema hayo ni masharti ya mganga.

Kama ulikuwa na tabia ya kulewa na kugawa fedha zako kwa watu, pale utakapoamua kuachana na ulevia na fedha ya pombe kuiweka akiba, watu watasema mke wako au mme wako kakuendea kwa wanganga. Kumbe mmefanya uamuzi wa pamoja wa kuhakikisha mnabadili haki yenu, maana ni mmeona ni ujinga kuwa mmepanga huku wewe ukitumia mshahara wote kwenye pombe tu.

Kiufupi nidhamu inaongea sana, bila nidhamu sahau kuhusu ndoto au hayo malengo yako.

Soma zaidi: Aina 5 Za Nidhamu Unazopaswa Kuwa Nazo

PIA ANGALIA VIDEO HII YENYE USHAURI MZITO KUTOKA KWA STEVE JOBS

Nne , ustahimilivu na zaidi adabu
Hiki Ni kitu kingine muhimu. Kustahimili ni kuchukua Mambo mazito bila ya kulalamika. Kustahimili ni kuwa na uwezo wa kubeba mambo mazito. Ni kuvumilia.
Kumbe unahitaji kuvumilia kabla ya kufikia ndoto yako yotote. Ebu fikiria umeweka ndoto ya kufikia uhuru wa kifedha. Hili lengo  halifikiki ndani ya siku moja. Linaweza kuchukua miaka kumi au ishirini. Sasa bila ya uvumilivu kwenye kipindi hiki, ujue wazi kuwa utakwama sana na hata kurudi nyuma. Hivyo, kumbe unapaswa kuwa mvumilivu.

Lakini pia tumeona kuwa safari hii ina vikwazo vingi sana, hivyo unapaswa kuwa mvumilivu unapopitia vikwazo na changamoto. Unapaswa kuwa mvumilivu pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo. Endelea kuwa mvumilivu.

Soma zaidi: Mo Dewji Afunguka Mazito Linapokuja Suala La Fedha.

Tano, Kutumia njia za mkato hazitakusaidia kufahamu au kufikia malengo kistahiki.
Kuna maneno ya kiingereza yanayosema, shortcuts will kill you. Au short cuts makes life shorter. Na ni ukweli. Njia za mkato zinaweza kukuua. Hivyo, epukana na njia zote ambazo watu wanasema kuwa hizi ni za mkato, badala yake chagua njia ambayo unaona wewe inakufaa na kisha endelea na hiyo.

Rafiki yangu, bila shaka huo ujumbe wa Mo Dewji kwako umeuelewa Sana. Chagua vitu vichache au hata kimoja ambacho unaona wazi kuwa unaenda kukifanyia kazi na kuhakikisha umekifanikisha.
Kazi yako leo iwe ni kuandika ndoto kubwa ya maisha yako
Andika hatua ambazo utaanza kuchukua hata kama ni ndogo ili uifikie hiyo ndoto yako.

Nakutakia kila la kheri rafiki yangu.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X