Njia 5 Za Kuifanya Fedha Ikufuate


 

Kuna watu wana tabia ambazo kwa vyovyote vile zinaendelea kuvuta fedha kwao. Na wengine kwa tabia yao, hata iweje Ni LAZIMA tu fedha iwakimbie. Umewahi  kujiuliza Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya fedha ivutike kwako mara kwa mara. Zifuatazo Ni njia tano za kuivuta fedha kwako.

1. TOA THAMANI KUBWA KWA WATU.

Labda kwanza ifahamike kuwa fedha zako wanazo watu mifukoni mwao. Na kwa vyovyote vile hawawezi kutoa hizo fedha na kukupa bila ya wewe kuonesha kuwa unastahili kupata hizo fedha. Hivyo, basi ni muhimu kwako kuonesha kuwa unastahili kulipwa fedha kwa kuanza kutoa thamani kubwa kwa watu. Hapo nayakumbuka maneno ya Zig Ziglar aliyesema unaweza kupata unachotaka kama utawasaidia watu kiasi Cha kutosha kupata Kile wanachotaka. Lengo la thamani ni kuwasaidia watu kupata kitu wanachotaka. Je, wewe upo tayari kutoa thamani kwa watu.

2. KUFANYA KAZI ZAIDI YA UNAVYOLIPWA

Kuna hadithi ya watu wawili. John na Bill ambao wanaajiriwa kwenye kampuni moja kwa wakati mmoja. John kila mara anafanya kazi yake bila ya kuongeza kitu cha ziada huku Bill akijituma na hata kufanya kazi zaidi ya vile inavyotegemewa kutoka kwake. Inafikia hatua ambapo Bill anapandiahwa cheo na John anaanza kulalamika.

Siku MOJA bosi anamwita John na kumtuma. Anamwambia akaangalie wateja wa bidhaa fulani kwenye eneo fulani. John alienda na baadaye akarudi na kusema wapo. 

Bosi wake anamwambia vizuri, ngoja Sasa nimtume ndugu yako Bill ili naye akaangalie, na wewe kaa hapa uone majibu atakayoleta. 

Bosi alimtuma Bill kwenye eneo lilelile, ili kuangalia wateja wa bidhaa hiyohiyo.

Baada ya muda Bill alirudi na kusema wateja wapo. Ila asilimia kubwa ya wateja hao ni wanaume, wenye umri kati ya miaka 18-55. Bill aliendelea kusema kuwa inavyoonekana bidhaa hiyo itauzika zaidi msimu wa kiangazi lakini ili kuiuza zaidi kwenye misimu yote tutpaswa kufanya marekebisho fulani kwenye bidhaa.

Hapo ndipo bosi alipomwambia John kuwa unaona tofauti kati yako na Bill? Na hiki ndicho kitu ambacho kinafanya Bill apandishwe cheo. Kumbe, Bill alikuwa anaenda hatua ya ziada kwenye kazi zake. Alikuwa anafanya zaidi ya vile alivyotumwa au vile inavyotegemewa kutoka kwake. Kitu hiki kilimwongezea sifa kazini.

Na wewe Unapaswa kujijengea utaratibu huu maishani mwako. Fanya zaidi ya UNAVYOLIPWA.

3. KUWA MBUNIFU NA FIKIRI NJE YA BOKSI

Kanuni inayofahamika Kama copy-cut principle inasema kwamba, ukianza kufanya biashara au kitu chochote hata Kama wewe ndiwe utakuwa ni mtu wa kwanza kwenye hicho kitu, watatokea watu wa kufanya kitu hichohicho ndani ya miezi sita. Hii ndiyo kusema kwamba unapaswa kuwa mbunifu kila mara na kufikiri jinsi ya kuwahudumia wateja wako vizuri kuliko mtu mwingine kwa sababu, nje ya hapo Kuna watu ambao wataanzisha kitu kama cha kwako na kuiga kile unachofanya, na hivyo utajikuta kuwa na wewe wateja wako wanapungua na hatimaye unatoweka kwenye biashara. Ila ukiwa mbunifu, hutaweza kutoka kwenye biashara kama kila mara utabuni njia bora za kuwafikia wateja wako, kuwahudumia na kuboresha huduma zako. (Nimeandika kitabu kuhusu ubunifu, ukikihitaji tuwasiliane)

4.  WAAMBIE WATU UTOFAUTI WAKO

Usemi wa wahenga waenda kwa kusema kuwa kizuri chajiuza ila kibaya chajitembeza. Hata hivyo Leo nataka nikwambie kuwa hata kizuri KINAPASWA kujitembeza. Huwezi tu kuwasha taa na kuificha chini ya kitanda ukitazamia imulike na watu waone mwanga wake. Unapaswa kuiweka juu ili iangaze vizuri. Vivyo hivyo, huwezi kutengeneza utofauti wako na kisha kutulia na kusubiri utofauti wenyewe ujitangaze. Utangaze wewe mwenyewe. Simama juu na toa sauti ukisema hapa ndipo ulioo ubora wa hali ya juu Sana.

Soma Zaidi: KONA YA SONGA MBELE: Nani Anakujua?

5. JITANGAZE

Coca-Cola ni kampuni kubwa sana, kiasi kwamba unaweza kufikiri hawahitaji kujitangaza tena. Maana soda yao tunaijua. Lakini cha kushangaa kila siku utaona tangazo lao  mtandaoni, au kwenye runiga, au njiani au utalisikiliza kwenye redio. Ila kiufupi, kila siku wanaendelea kujitangaza wao na bidhaa yao bila kuchoka.

Na wewe Unapaswa kufanya hivyo pia kila siku.

Unaweza pia kupenda  NGUVU YA KIDEO NA UNAVYOWEZA KUITUMIA KUONGEZA MAUZO

Nguzo Tano Za Masoko

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X