Njia Tano Za Kujitofautisha Mwenyewe Kwenye Kile Unachofanya


Tunaishi katika dunia ambapo watu wengi wanapenda ufanye mambo kwa namna ya kawaida. Upate metokeo ya kawaida na kuishi maisha ya kawaida. Hata kama utasema kwamba hutaki maisha ya aina hii, utajikuta kwamba unalazimika kuishi maisha ya kawaida kwa sababu kila mtu kwenye jamii anafanya hivyo. Na ikumbukwe kuwa watu waliokuzunguka wana nguvu kubwa ya kukuvuta wewe ili uishi Kama wao . Hivyo basi, usipozijua njia za kujitofautisha. Ni wazi kuwa lazima tu kwenye hii dunia utaishi maisha ya kawaida sana.

Hii ndiyo kusema kuwa NDOTO, malengo na mambo yote makubwa unayopanga kufikia, hutayafikia kwa sababu tu, unaishi maisha ya kawaida. Sasa ili kuondokana na hali hii, unapaswa kujitofautisha na walio wengi kwa kufanya yale yanayofanywa na wachache. Na yenyewe ndiyo haya hapa;

1. Kuweka malengo
Ni asilimia 3 tu ya watu wenye malengo maishani mwao. Hivyo na wewe ukiweka malengo yako utakuwa umejiweka kwenye hii jumuiya ya watu wachache. Ila hii asilimia tatu ya watu huwa inafikia mambo makubwa ambayo watu wengi huwa hawafikii maishani mwao. Jitofautishe mwenyewe kwa kuanza kuweka malengo leo.

Soma Zaidi; JINSI YA KUWEKA MALENGO

2. Fahamika kama mtu wa vitendo.
Nakumbuka o-level tulikuwa na jamaa darasani alikuwa anapenda sana kuongea. Angeweza kukutisha (au kukupiga mkwara) kuwa atakupiga na kukuumiza vibaya sana. Kwa vitisho vyake tu, ungefikiri jamaa ana nguvu kuliko watu wote hapa duniani.

Lakini baadaye ilikuja kugundulika kuwa huyu jamaa hakuwa hata na nguvu za kugombana ila alikuwa mtu wa maneno mengi na alikuwa hawezi kumpiga mtu.

Sasa kwenye maisha ya kawaida Kuna watu wengi pia ambao wanaongea. Wanaongea kuwa watafanya kitu fulani, watatembelea nchi fulani n.k.. Sasa njia ya wewe kujitofautisha kutoka kwenye kundi la hawa watu ni kuhakikisha wewe unakuwa mtu wa vitendo. Ongea kidogo ila tenda sana. Vitendo vinalipa kuliko maneno.

Siku moja Diamond Platnumz alikuwa anahojiwa kuhusu watu wengine wanaosema kuwa wana vipaji na uwezo kuliko yeye. Alisema, mimi sitaki maneno. Anayesema ana uwezo kuliko mimi aoneshe huo uwezo kwa vitendo na wala siyo maneno.
Nakusihi sana na wewe rafiki yangu kuwa ujenge utaratibu wa kuongea kidogo, ila kutenda sana.

3.  Bobea kwenye kitu fulani
Kwenye mtandao wa Quora Kuna mtu aliuliza, nawezaje kuwa Kama Elon Musk, Jeff Bezos au Bill Gates?  Justin Musk ambaye ni mke wa Elon Musk, alijibu kwa kusema HUWEZI. Ila kama unataka kufikia kwenye viwango walivyofikia basi chagua kitu kimoja kisha bobea kwenye hicho kitu kiasi kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kubobea kwenye hicho kitu kama wewe. Kisha baada ya hapo bobea kwenye kitu kingine. Mfano, bobea kwanza kwenye uhasibu kisha bobea kwenye kompyuta. Baada ya hapo unganisha hivyo vitu viwili kutengeneza kitu kimoja.

Alimalizia kwa kusema, uliweza kufanya hivyo, nakuhakikishia hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kukufikia kwenye kitu utakachofanya.

Sasa na wewe Unapaswa kubobea. Dunia ya leo bado inawapenda sana wabobevu na inawalipa vizuri ukilingamisha na watu wa kawaida.  Sasa swali langu kwako, unaemda kubobea katika nini?

Kama ungependa kubobea kwenye uandishi hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Bonyeza hapa.

4. Jitangaze Mara kwa Mara
Tunaishi kwenye ulimwengu wenye kelele nyingi sana. Watu wanashindwa kuweka nfuvu zao sehemu moja kutokana na wingi wa kelele, mitandao ya kijamii inawavuta huku na kule, hivyo watu hawatulii. Sasa Kama unataka kujitangaza au kutangaza bidhaa yako kwenye hii dunia ambayo ina kelele nyingi haupaswi kufanya hivyo mara moja,

Saikolojia inaonesha kuwa watu wakikusikia mara ya kwanza hawafuatilii chochote, wakikusikia mara ya pili inakuwa bado. NI mpaka pale wanapokusikia au kusikia bidhaa yako walau kuanzia MARA SABA, ndio wanaanza kuchukua hatua. Kwa hiyo,  basi, usitangaze bidhaa au huduma au kuonesha uwezo wako Mara moja. Fanya hivyo Mara nyingi kadiri uwezavyo.

4. Usijilinganishe na watu wengine
Mwanzoni kabisa tumeona kuwa unapaswa kuepuka kuishi maisha ya kawaida maana haya maisha hayalipi. Na moja ya kitu kitakachokupelekea uishi maisha ya kawaida ni kujilinganisha na watu wengine. Usifanye vitu wanavyofanya wengine kwa kuwaiga ili uwe kama wao. Amua tu kuanza kuishi maisha yako, basi. Na Wala siyo chini ya hapo.

Mtu pekee unayeweza kujilinganisha naye ni wewe wa jana au mwaka jana. Ili kuepuka kujilinganisha na watu wengine, jua wapi unaenda, na nini unataka maishani.

5. Jifunze
Jenga utaratibu wa kujifunza Mara kwa Mara. Utaratibu huu utaweza kukusukuma mbali na kukusaidia wewe kufanikisha makubwa.  Jifunze kupitia kusoma vitabu, Soma vitabu Kama vile maisha yako yanategemea kusoma vitabu. Kuna mengi kwenye vitabu ambayo yatakusaidia wewe kufika mbali. Na ukweli kuhusu kusoma vitabu ni kuwa ukisoma kitabu chukua walau kitu kimoja na ukifanyie kazi. Pia, hakikisha unaweka katika vitendo Yale unayosoma. Usiishie tu kusoma vitabu, Soma vitabu na weka kwenye vitendo yale unayojifunza.

Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X