Vitabu ni mojawapo ya njia ya kuongea na watu waliofanikiwa, viongozi maarufu, wanafalsafa, na hata watu wengine ambao tayari walishaaga dunia. Ni kupitia usomaji wa vitabu ndipo tunapata kuongea nao, kusikiliza maoni yao na hata kujadiliana nao mada fulani fulani.
Sasa, watu wengi huwa hawapendi kusoma vitabu kutokana na ukweli kuwa vitabu vingine ni vikubwa sana kwa umbo na wengine basi tu hawajejenga tabia ya kusoma vitabu. Tayari nimeandika kitabu kizima kuhusu usomaji wa vitabu. Unaweza kupata bure nakala yako kwa kuwasiliana nami kupitia 0755848391
Sasa siku ya leo ningependa kukuonesha njia tano zitakazokufanya wewe hapo kuanzisha tabia ya kusoma vitabu Vikubwa na kuvimaliza.
Moja, hakikisha umechagua kitabu unachotaka kusoma.
Pili, kijue kitabu chako kina kurasa ngapi?
Tatu, jipe muda utakaoutumia kukisoma. Kama ni wiki, au mwezi. Kisha gawa idadi ya kurasa kwa idadi ya siku utakazotumia kukisoma. Kama kitabu kina kurasa 300. Na wewe ungependa kukisoma kwa mwezi mmoja, hiyo ni sawa na kusoma kurasa 10 kila siku.
Nne, Anza kusoma Idadi ya kurasa husika kila siku. Fanya hivyo asubuhi na mapema sana kabla akili haijachoka.
Tano, Rudia hatua ya kwanza mpaka ya nne kusoma kitabu kingine.
Rafiki yangu hizo hapo ndizo njia tano na rahisi za kusoma vitabu. Kila la kheri.
Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391