Njia Tano Za Kuyafanyia Kazi Malengo Yanayojirudia Kila Mwaka


Kuna malengo ambayo huwa yanajirudia kila mwaka. Yaani, utakuta kuwa kila mwaka lengo hilohilo linajirudia na linapaswa kufanyika. Na tena unaweza kukuta lengo la aina hii linahitaji fedha. Zifuatazo ni njia tano za kufanyia kazi malengo Yanayojirudia kila mwaka.

Kwanza, yafahamu malengo yenyewe Yanayojirudia kila mwaka. Kama Ni kusafiri kwenda kuwaona wazazi, kupanda miti, kuchapa kitabu n.k.

Pili, Fahamu kama lengo lako linahitaji fedha kutimia au linahitaji rasilimali nyingine kama muda kutimia.
Mfano, kupanda kiti 100 kila mwaka ni lengo linalohitaji fedha wakati kuandika na kuchapisha ebook (nakala laini) Ni lengo linalohitaji rasilimali muda.

Tatu, Kama lengo lako linahitaji fedha Anza kuweka akiba kuanzia mwanzoni mwa mwaka. Na uwe mtu wa kuweka akiba kwa uendelevu bila kuacha hata baada ya kulikamilisha kwa mwaka huo, endelea kuweka akiba kwa ajili ya maandalizi ya mwaka unaofuata.

Kama lengo linahitaji rasilimali nyingine, Basi angalia jinsi utakavyolipatia rasilimali hiyo ili kufanikisha lengo lako.

Nne,  Kwa lengo linalohitaji fedha litengenezee chanzo chake cha fedha Cha kudumu. Hiki kinakusaidia wewe kujua mara zote kuwa lengo fulani chanzo Cha fedha ni sehemu fulani. Kufikia hapa ni wazi kuwa utakuwa pia unefungua akaunti ya kudumu ambayo utakuwa unaweka hiyo fedha.

Tano, jifanyie tathmini kila mwezi. Kwa malengo haya yanayojirudia kila mwaka. Hakikisha kila mwezi unafanya tathimini na kuona umetoka wapi, uko wapi na unaenda wapi. Kila Mara jikumbushe kwa nini uliweka lengo hilo na kwa nini mwaka huo Ni LAZIMA ulifanikishe hilo lengo.

Rafiki yangu, hizo hapo ndizo Njia Tano Za Kuyafanyia Kazi Malengo Yanayojirudia Kila Mwaka. 

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


One response to “Njia Tano Za Kuyafanyia Kazi Malengo Yanayojirudia Kila Mwaka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X