Kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, ni kitabu ambacho kimeeleza kwa kina jinsi wewe unavyoweza kufanikisha NDOTO ZAKO na kufanya mambo makubwa. Kitabu hiki kina madini kuanzia mwanzo wa kitabu mpaka mwisho wa kitabu. Sasa kwenye hiki kitabu kuna nukuu nyingi ambazo zimekonga nyoyo za watu, ila leo nitakushirikisha nukuu tano tu.
1. …Ukweli ni kwamba mimi ninakudai. Ndiyo ninakudai. Ninakudai biashara hiyo unayoifikiria kuanzisha miaka nenda, miaka rudi ila unasita kuanzisha. Ninakudai bidhaa hiyo uliyokuwa unafikiria kutengeneza, ila hujaanza kutengeneza, ninakudai kitabu chako hicho, ninakudai igizo lako hilo. …ninaomba ulipe deni langu kwa kuanza kufanyia kazi NDOTO yako.
Nimeandika hivi nikiwa naeleza ni kwa jinsi gani watu huwa wanakufa na vitu ambavyo vingeweza kuwa msaada kwetu na hata kutusaidia kukamilisha malengo yetu. Siku ya leo naandika makala hii kwa kutumia simu janja (smartphone) kwenye app ya simplenote. Binafsi namshukuru aliyetengeneza simu na app hii maana wamenirahisishia utendaji kazi, lakini pia wananifanya nitimize ndoto yangu ya uandishi.
Kumbe laiti hawa watu wasingekuwa wametimiza wajibu wao, mimi sasa hivi ningekuwa nahangaika kuandika. Pengine ningekuwa naandika kwenye daftari, au ningekuwa siandiki kabisa. Na hilo lingekuwa deni kubwa sana. Lakini pia Mimi nimeshapata hiki kifaa, napaswa kukitumia kwa manufaa ili na mimi nichangie kwenye kuwasaidia watu zaidi kufikia NDOTO ZAO.
Kumbe kwa ndoto yako hiy, inawezekana wewe umeshikilia ajira za watu. Inawezekana ukitimiza ndoto yako hiyo, ukawafanya wengine watimize ndoto zao pia.
2. Kitu muhimu cha kufahamu Ni kuwa watu wananunua jina. Kama huamini toa wiki moja ambayo kwa watu utajitambulisha kama Yuda Isikarioti, halafu uone watu watakavyoupokea huo utambulisho wako.
Jina, jina, jina. Jina ni muhimu sana. Unapaswa kujijengea jina zuri. Jina baya litakufanya ukose mpaka fursa.
3. Siyo kila mtu anapaswa kuambiwa apumuzike kwa amani pale anapoaga dunia. Kwa Nini? Kwa sababu Kuna wengine walipumzika hapa duniani.
Hii imekuwa ni imani yangu ya siku nyingi sana, hii ni kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanalala sana, badala ya kufanyia kazi NDOTO ZAO. Lakini bado siku wakifa tunawaambia wapumzike kwa amani. Wapumzike mara ngapi? Walipumzika hapa duniani na bado wanaenda kupumzika kwenye ulimwengu ujao!
4. Watu wenye kichaa cha kutosha kiasi Cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia, ndio ambao huibadili -Steve Jobs
Hii ni nukuu ya Steve Jobs akiwa anasisitiza kuwa watu wengi ambao huwa wanaamua kufanyia kazi NDOTO ZAO, mwisho wa siku huwa wanaonekana kama vichaa. Ila siyo wote wanapenda kuonekana vichaa, ndio maana wengine huwa wanaaacha kufanyia kazi NDOTO ZAO kwa uoga wa kuonekana vichaa. Hata hivyo, Steve Jobs anasema kuwa, watu wenye kichaa cha kutosha kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia ndio ambao huibadili.
Kumbe pale watu wanaposema huyu ni kichaa, wewe ukaamua tu kuwa kwa vyovyote vile, lazima nisonge mbele na kufanikisha NDOTO zangu, hapo utakuwa umeendelea kuwatangazia watu kuwa u kichaa. Ila siku zote watu wenye kichaa cha kutosha, kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia, ndio ambao huibadili.
Maneno haya aliyasema Steve Jobs mwaka 1997 kwenye tangazo la kampuni yake ya Apple la Think Different. Kwenye tangazo hilo alitolea mifano ya watu walioonekana vichaa kwa jamii ila wakafanya Mambo makubwa. Watu kama Albert Einstein, Thomas Edison, Richard Branson, Henry Ford na wengineo. Sasa je, wewe una hata ka kichaa kidogo?
5. Ukitaka kung’aa kama jua, kuwa tayari kuungua kama jua. AP.J Abdul Kalam
Jua linang’aa sana. Bill shaka na wewe ungependa kung’aa kama jua. Ila siri ya kung’aa kwa jua ni kuungua. Bila kuungua hakuna kung’aa. Na wewe ukitaka kula vinono basi kuwa tayari kuungua. Kwenye kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, sura ya tano yote inaeleza kiundani kuhusu gharama ambazo wewe unapaswa kulipa ili kutikia ndoto zako. Kulipa gharama hizi ni sawa na kuamua kuungua. Lakini unakuwa umeamua kuungua ili upate vinono hapo baadaye. Ukipata nakala ya kitabu hiki utajifunza mengi kuhusu ulipaji wa gharama. Wasiliana nami sasa kwa 0755848391. Kumbuka; ukitaka kung’aa kama jua basi kuwa tayari kuungua kama jua.
NUKUU YA NYONGEZA
6. Unaweza kuwa na meli bora sana, na ukawa na nahodha mzuri kuliko wote duniani, ila Kama haujui unaelekea wapi, ujue utazunguka huku na huko ila mwisho wa siku hautafika sehemu ya maana. Arnold Schwarzenegger.
Kumbe! Unaweza kuwa na rasilimali za kila aina, ila usipojua unazitumia kwa ajili ya kufanya kitu gani. Ujue mwisho wa siku rasilimali hizo hazitakusaidia. Kuna picha fulani ilikuwa inaonesha mtu ambaye alikuwa na ngazi nyingi, lakini alikuwa anahangaika kuona ng’ambo ya pili. Kumbe haitoshi tu kuwa rasilimali bila kujua namna ya kuzitumia. Na haitoshi tu kujua namna ya kuzitumia, unapaswa kujua unazitumia ili mwisho wa siku zilete matokeo gani.
Hizo hapo rafiki ndizo nukuu tano na moja ya nyongeza, Zilizokonga Nyoyo Za watu kutoka kwenye kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kitabu hiki ni mahsusi kwako wewe mwenye ndoto.
Kupata nakala ya kitabu hiki, wasiliana na na 0755848391. Nakala ngumu (hardcopy) inapatikana kwa 20,000/-
Na nakala laini gharama yake ni 15,000/-
Karibu sana.
Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391
kila la kheri