Sababu 5 kwa nini unashindwa kufanikisha malengo unayoweka


Najua. Umekuwa unaweka malengo mara kwa mara ila unashindwa kuyatimiza. Zifuatazo ni sababu tano (05) zinazokukwamisha wewe kutimiza malengo yako. Sitaishia tu kukuonesha sababu hizi bali pia nitakueleza kiundani namna ya kuepukana na sababu hizi ili uweze kufanikisha malengo yako..

Moja, NI KWA SABABU UNAWEKA MALENGO MENGI KWA WAKATI MMOJA.
Una Mambo mengi ambayo ungependa kufanikisha, hivyo unajikuta kwamba unataka kuyafanya yote kwa wakati mmoja. Hata kama malengo yako yatakuwa mazuri kiasi gani, bado hii itakuchosha sana. Itakufanya ugawe nguvu, rasilimali zako (muda, fedha na hata akili) kwenye maeneo tofauti tofauti na hivyo kushindwa kuweka nguvu kwenye kitu kimoja na hata kukutatisha tamaa

Ili uweze kuyafanikisha malengo yako vizuri unapaswa kuweka lengo moja kwa wakati, kulifanyia kazi na kulitimiza kabla ya kufanyia kazi lengo linalofuata.
Hii itakusaidia kupata nguvu unapokamilisha lengo moja kwenda jingine.
Kufocus kwenye kitu kimoja kwa wakati
Kuweka rasilimali zako sehemu moja na hivyo kufanya makubwa tofauti na pale unapozigawa hovyohovyo.

Unaweza kufanikisha lengo moja kwa wakati Kama;
1. Utayawakea vipaumbele malengo yako. Unakuwa na lengo la kwanza, la pili na kuendelea. Unapoanza kufanyia kazi unafanyia kazi lengo la kwanza kabla ya mengine.

2. Fahamu kuwa una muda kidogo, hivyo haupaswi kuugawa kila sehemu hata kwenye mambo yasiyo na msingi.

3. Lakini kwa malengo yanayoendana yanaweza kuwekwa pamoja ili kuepuka kuwa na malengo mengi.

Pili, UNAKAA SANA NA WATU WANAOKUKATISHA TAMAA
Watu wanaokatisha tamaa wanaweza kukufanya ushindwe kutimiza malengo yako. Kila mara watakuwa wanakwamvia haiwezekani, utaweza kufanikisha lengo fulani kama nani? Haijawahi kufanyika. Watu wa aina hii kila mara huongelea mambo hasi na Mambo yanayoonesha kuwa haiwezekani.

Tafiti zinaonesha kuwa mtu mmoja akikwambia haiwezekani basi wanahitajika watu 17 kukwambia inawezekana. Ukweli ni kwamba kuwapata watu 17 wa kukupa moyo ni nadra sana. Hivyo, jiepushe kadiri uwezavyo na watu wanaokatisha tamaa.

1. Jenga urafiki na vitabu
2. Marafiki wazuri na
3. Sikiliza mafunzo mazuri mitandaoni

Tatu, HAUCHUKUI HATUA BAADA YA KUWEKA MALENGO YAKO.

Kuweka malengo bila kuchukua hatua haitoshi. Unapaswa kuwa mtu wa kuchukua hatua kila unapokweka malengo. Yafanyie kazi bila kurudi nyuma mpaka yatimie. Jipe muda wa kufanyia lengo husika kulingana na aina ya malengo uliyoweka.

Nne, UNAAZA kUFANYIA MALENGO YAKO ILA UNAISHIA NJIANI.

Hii ndiyo kusema kwamba sababu nambari tatu unaweza kuivuka ila ukianza kufanyia lengo lako unaishia njiani. Ili kuepuka hili,
Hakikisha hauwi na malengo mengi Kama ambavyo tumeshasema.
Pia, hakikisha unaazimia kuchukua hatua hata kama ni ndogondogo  kila siku mpaka lengo ulifikie.
Usikubali kamwe kuishia njiani. Fahamika kama mtu ambaye huanzisha vitu na kuvikamilisha.

Tano, HAUNA SABABU ZA KUTOSHA ZA KUFANIKISHA LENGO LAKO


Kwa nini unataka kuweka akiba ya milioni 100? Kwa nini unataka kupungua uzito? Kwa nini una lengo la kufanya mazoezi? Kama hauna sababu kubwa kwa lengo, utalifanya na kuishia njiani. Hivyo basi kwa kila lengo unaloweka hakikisha una sababu za kwa nini linapaswa kutimia. Sababu hizi zitakufanya usonge mbele hata Kama unakwama.

SOMA ZAIDI: Vitu Nane (08) Vidogo Ambavyo Unaweza Kuanza Kufanya Leo, Vikaongeza Thamani Yako Na Ya Watu Wengine


Sita, SABABU YA NYONGEZA: UNATAKA KUWARIDHISHA WENGINE.

Kama unaweka malengo kwa ajili ya KUWARIDHISHA WENGINE, itakuchosha pia na hata itakufanya ka ushindwe kufanyia lengo lako kikamilifu. Maana kila mara utakapokuwa umeanza kufanyia kazi lengo hilo la KUWARIDHISHA WATU, kitatokea kingine ambacho utaona kinafaa KUWARIDHISHA WENGINE kuliko kile Cha mwanzo. Kwa hiyo, wewe kila wakati utakuwa tu ni mtu wa kutafuta KUWARIDHISHA WENGINE kwa kufanya kila kinachotomea na kuacha na kwenda kwa kingine.

Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri
One response to “Sababu 5 kwa nini unashindwa kufanikisha malengo unayoweka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X