Sababu tano kwa nini hufanikiwi


 

Unaendeleaje rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii nyingine mpya na ya kipekee sana. Siku ya leo ninaenda kukushirikisha sababu tano, kwa nini wewe hapo hufanikiwi. Kwenye kila sababu tunaenda kuona ni kitu gani ambacho wewe unaweza kufanya ili na wewe uweze kuingia kwenye orodha ya watu ambao wamefanikiwa. Hivyo, kaa mkao wa kula maana ndio kwanza safari yetu imeanza.

 

MOJA, HUFANIKIWI KWA SABABU UNAFANYA MAMBO MENGI KWA WAKATI MMOJA

Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni miongoni mwa kitu kinachofelisha watu wengi sana kwenye maisha. Hii ni kutokana na ukweli kuwa unapofanya mambo mengi kwa wakati mmoja unajikuta kwamba unagawanya nguvu zako huku na kule huku ukishindwa kuweka nguvu zako sehemu moja na yenye manufaa kwako.

 

Kinachofanya watu wagawe nguvu na muda wao ni kwa sababu ya wingi wa fursa hasa kwenye zama hizi hapa. karibia kila siku kuna fursa mpya ambayo ni lazima tu utaisikia watu wakiwa wanaisema, leo hii utasikia kwamba kuna fursa fulani, na kesho utasikia kuwa kuna fursa nyingineyo. Sasa ukiwa mtu wa kuchangamkia kila fursa inayokuja mbele yako, inamaanisha kwamba utashindwa kuweka nguvu zako sehemu moja na hivyo, kujikuta kwamba umejifelisha mwenyewe. Hutafahamika kama mtu anayefanya kitu fulani.

 

Kitu muhimu ambacho wewe unapaswa kufanya ni kuhakikisha kwamba unachangua kitu kimoja na kukifanya hicho kwa nguvu zako zote. Kifanye hicho kitu bila kujali mbele yako kunatokea fursa nyingine zipi. Na hata zikitokea hizo fursa, kwa sasa hivi achana nazo, wewe endelea kuweka nguvu zako kwenye hicho kitu kimoja ulichochagua mpaka ukifanikishe.

 

 

PILI, HUJITUMI HASWA

Usipokuwa mtu wa kujituma, maana yake utakuwa ni mtu wa kufanya kazi kidogo na kisha kuacha.  Ukishachagua kitu kimoja unapaswa kuhakikisha kwamba unakiwekea nguvu na unakifanya kwa kujituma haswa bila kuacha bila kujali kinatokea nini. endapo utaamua kufanya hicho kitu bila kujali kinatokea nini, nakuhakikishia kuwa siku moja watu wataanza kusema aisee, tulikuwa tunaona kama unacheza vile kumbe ndio ulikuwa umeamua. Aisee, aisee, aisee. Yaani, hizo aisee zao zitakuwa hazielezeki ila kumbe wewe ndiyo utakuwa umefanikisha hiho kitu.

 

TATU,UNAPENDA STAREHE KULIKO UNAVYOPENDA KUFANIKIWA

Ebu fikiria, eti unapenda kufanikiwa halafu eti bado unajihusisha na vijitabia kama kuvuta sigara, bangi, kunywa pombe na vinginevyo. Hivi vitu vinaenda kukukwamisha na kukuangusha chini rafiki yangu. Kama bado unajihusisha na vijitabia vya aina hiii unapaswa kuamua kuachana navyo ili uweze kusonga mbele na kufanya mambo yako mengine. Hivi vitu unaaweza kuviona vidogo, ila vitaendelea kuwa mwiba kwako na kwa mafanikio yako.

 

NNE, UNAPENDA KUIGA VITU WANAVYOFANYA WENGINE

Wewe. Ndiyo wewe unapenda kuiga vitu wanavyofanya watu wengine ili uweze kuwa kama wao. Hauoneshi ule uhalisia na ukweli wako. Badala yake unataka kufanya kama fulani anavyofanya. Ninachopenda kukwambia ni kwamba huwezi kuiga na kufanya kama anavyofanya mtu fulani huku ukitegemea kupata kile kitu ambacho na yeye amepata. Kama unataka kufanikiwa basi chagua eneo lako ambalo wewe mwenyewe utabobea na bobea huko. Huwa napenda kuwaambia watu kuwa Bill Gates ajaye siyo kwamba atakuwa atatengeza softwares kama huyu tunayemfahamu. Wewe hapo unaweza kuwa Bill Gates kwa kufanya kilimo, au kwa kutumia kipaji chako, ujuzi au elimu yako. Ila usiige na kufanya kilea kitu wanachofanya wengine. Kuwa wewe.

 

TANO, HUJASOMA KITABU CHA AKILI YA DIAMOND

Kitabu hiki ni kidogo sana, ila ni kitabu chenye mambo yatakayokusaidia kufikia mambo makubwa sana. Kitabu hiki ambacho kimeleta masomo muhimu ya kimaisha kutoka kwa mwanamuziki Diamond Platimumz kinatushirikisha mambo 50 kutoka kwa mwanamuziki huyu. Ila mambo haya ni yenye nguvu kubwa sana, kiasi kwamba kama utayafanyia kazi ni lazima tu siku moja utafika mbali.

Vitu vyote vilivyo kwenye kitabu hiki hapa tunaweza kuvigawa kwenye vipengele vitatu, KIPAJI, UBUNIFU na MAFANIKIO. Unaenda kujifunza kuhusu kipaji moja kwa moja kutoka kwa Diamond Platinumz, unaenda kujifunza kuhusu ubunifu moja kwa moja kutoka kwa Diamond na hatimaye utajifunza mafanikio kutoka kwake pia. Hiki ni kitabu ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba unacho na umedhamiria kukisoma bila ya kurudi nyuma.

 

Rafiki yangu,hayo ndiyo mambo matano ambayo yanakufanya wewe hapo usifanikiwe mpaka sasa hivi. yabadilishe hayo na maisha yako yatabadilika. Kila la kheri.

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X