Ushauri wa Aliko Dangote Kwa Kijana Anayetaka Kuanzisha Biashara


Aliko Dangote ni tajiri namba moja kwenye bara zima la Afrika, kitu kikubwa ambacho kimemfanya yeye kuwa tajiri mkubwa ni biashara zake anazofanya. Amekuwa akifanya biashara tangu miaka ya 70 mpaka leo.

Ameanzia chini (SIFURI) mpaka ameweza kufikia mafanikio makubwa (KILELENI). Hivyo, ni wazi kuwa lazima  atakuwa na busara za kumwaga kwako na kwangu linapokuja suala zima la biashara. Kwanza kutokana na wingi wa miaka aliyotumia kwenye biashara. Pili, kutokana na ukweli kuwa kafanikiwa kwenye biashara alizofanya. Hivyo, busara zake zitakuwa za manufaa sana.  Ndio maana leo nimeona nimlete kwako ili uweze kujifunza kwake kitu kikubwa Sana, hasa wewe unayependa kuanzisha biashara au ambaye tayari una biashara.

Aliko Dangote anasema kwamba, kwa kwa biashara yotote ile unayoamua kufanya, hakikisha unaifahamu hiyo biashara nje ndani. Jifunze kila kitu kuhusu hiyo biashara. Haifai kuingia kwenye hiyo biashara ukiwa hujui kila kitu. Na hata ikitokea umeingia kwenye biashara bila kujua kila kitu, basi unapaswa kuweka mkakati wa kujifunza na kuijua hiyo biashara nje ndani.

Hata kama tayari umeanza biashara, weka mkakati wa kuijua biashara yako kiundani. Kiufupi,  unapaswa kuwa na mpango endelevu wa kujifunza na kuielewa biashara yako. Hiki ni kitu ambacho kitakutofautisha wewe pamoja na watu wengine watakaoamua kujihusisha na hiyo biashara.

Unaweza pia kusoma: Mo Dewji Afunguka Mazito Linapokuja Suala La Fedha.

TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita (06)Za Kukutana Na Watu Maarufu, Wafanyabishara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X