Vitu Vitano vya kuepuka ili uweze kufikia malengo yako


 

Ni wazi kuwa furaha ya mtu yeyote anayeweka malengo ni kuona yanakamilika. Kama umeweka malengo yako kwa kufuata VIGEZO sahihi na kuepuka HAYA ni wazi kuwa malengo yako yatatimia. Hata hivyo, malengo yako yanaweza yasitimie kutokana na wewe kuendekeza vijitabia vingine vya kukukwamisha. Hivyo, hapa chini kuna vijitabia vitano unavyopaswa kuepuka baada ya kuweka malengo.

Soma zaidi: Hatua Saba Muhimu Katika Kuweka Malengo

1. Epuka kuweka malengo na kusali tu bila kufanya kazi
Kuna watu wakiweka malengo, kinachofuata ni wao kusema wanamwachia Mungu. Hawafanyi chochote ila wanabaki tu kusema Mungu atasaidia. Unachopaswa kufanya ni kuwa Mungu anasaidia wanaojisaidia.

2. Kubaki chumbani bila kufanyia kazi malengo yako
Huwezi kufanikisha malengo yako ukiwa chumbani umelala. Ukiweka malengo, amka kisha ingia kwenye ulingo wa kufanyia kazi malengo yako. Malengo bila kuweka kazi ni kazi bure. 

3. Kutojiamimi kama vile malengo hujayaweka wewe, badala yake yamewekwa na mwingine. Ukiweka malengo yako unapaswa kujiamini na Kuyafanyia kazi hata kama kuna wengine wanaokukatisha tanaa.

4. Kufuatilia Malengo/maisha Ya Watu wengine

Ukishaweka malengo yako, achana na kufuatilia maisha na malengo ya watu wengine. Wewe mwenyewe fuatilia malengo yako. Mambo ya nani anaishi wapi na yupo na nani, achana nayo.

Weka nguvu zako, muda wako na akili zako kwenye malengo yako tu.

5. Epuka kusubiri mpaka mwisho wa mwaka ili uanze kufanyia kazi malengo yako. Kuna watu wengi huwa wanaweka malengo na kisha kusubiri mwisho wa mwaka ili wafanyie kazi malengo yao. Hata hivyo, haipaswi kuwa hivyo. Malengo yako yanapaswa kufanyiwa kazi kila siku. Ukiyafanyia kila siku baada ya mwaka utakuwa umefika mbali Sana. Hatua moja moja  kila siku baada ya mwaka zinakuwa hatua kubwa sana.

Rafiki yangu, hivyo ndivyo vitu Vitano vya kuepuka ili kufikia malengo yako.

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391
One response to “Vitu Vitano vya kuepuka ili uweze kufikia malengo yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X