JINSI ya kunufaika na blogu kwa kazi yako unayoifanya.


Jana juna mtu alinifuata inbox na kuniuliza swali hili hapa.

Kaka , salama ? Mimi nawezaje kunufaika na blog kazi yangu ni mhubiri neno la Mungu

Ujimbe niliomjibu naamini utakuwa wa msaada kwako pia nilimjibu hivi.

1. Mahubiri yako yatakuwa hewani na kutuzwa. Kitu ambacho kitawasaidia wasomaji wako hata ambao hawakujui kuweza kuyasoma kwa wakati wao.

2. Dunia ya sasa imebadilika. Mtu akiwa na shida yoyote ile anakimbilia kukitafuta mtandaoni, hata mahubiri!

Huwezi amini siku moja kuna mtu anaweza kutafuta mahubiri yako na akayasoma au kuyasikiliza na wewe ukaokoa roho yake kwa njia hiyo.

3. Unaweza kuandika kitabu chako taratibu huku ukiwa na uhakika kuwa haupotezi kazi yako yoyote uliyoweka kwenye blog.

Mfano mzuri ni mimi hapa. Nimeanza kuandika September 2016, ila mpaka Leo naandika.
Cha kushangaza sijapoteza kazi za septemba 2016. Zimejaa tele kwenye blogu yangu. Nikihitaji kuzifanya kitabu naweza kufanya hivyo.

Lakini leo hii Kuna watu wamesoma kazi yangu ya 2016 na wamefurahi kuwa kazi hiyo imewabariki na kesho watakuwepo WENGINE pia.

Hii Ni kutokana na ukweli kuwa kazi hizo zipo hewani muda wote na  kazi yake ni kuwasaidia watu kihivyo.

MAKALA YANGU YA OKTOBA 2016 HII HAPA

Hii Ni miongoni mwa makala zangu za kwanza kabisa kuandika mwaka 2016, ila mpaka Leo hii ipo hewani tu inadunda.πŸ˜€πŸ˜€

Labda niamua mwenyewe kuitoa hewani.

Lakini pia inanisaidia kuona ukuajo wangu kwenye uandishi. Kadiri ninavyokua, ninarejea huku Mara moja moja na kusema nilianzia hapa ndio maana niko hapa. Hapa nilikuwa mchicha, Sasa ninakuwa mbuyu

4. Zipo faida nyingine nyingi.
Ikiwa ni pamoja na kuongeza kipato chako. Maana blogu yako hailali, ukiweka tangazo muda woote, saa 24 yenyewe inafanya kazi ya kulionesha mpaka ukiamua kulitoa mwenyewe.

Watu wakisoma kazi zako kwenyw blogu wataanza kukuuliza, baba mchungaji huna kazo nyingine? Nawe utawaambia mkitaka zaidi nimeandika vitabu, au kuna mahubiri ya kila jumapili kwenyw majarida tafadhali yanunuenu, nao watakuwa tayari kuyanunua

Na hapa nimeeleza kwa ufupi ila ndo hivyo..

5. FAIDA NYINGINE NI KUWA BLOGU Ni sehemu ya wewe kuonesha ujuzi wako.

Kama wewe ni Mwandishi na unataka kupata nafasi ya kuandika kwenye magazeti au sehemu nyingine, kitu cha kwanza watakuuliza, una ujuzi wowote?

Na wewe utaitikia naam, nina ujuzi wa kutosha tu. Nimekuwa naandika kwenye blogu yangu kuanzia mwaka….mpaka leo hii. Jioneeni wenyewe hapa…(hapo utawawawekea link yako ya blogu na kukaa pembeni, nakwambia watakutafuta kama mtoto aitafutavyo pipi au andaziπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€).

Nilipata nafasi ya kuandika kwenye gazeti la mwananchi hivihivi!

Ona picha hapa chini

Gazeti la mwananchi liliniuliza una uzoefu wowote kwenye masuala ya uandishi, nami niliwajibu, naam, ninao. Na ushahidi Ni blogu yangu,
Nilipowatumia makala chache, walikuwa tayari kuchapa kazi zangh kwenye gazeti lao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X