Kama huoni pa kuanzia kabisa ili kupata fedha Basi Anza


1. Kwa kutumia nguvu zako (fanya kazi kutumia nguvu zako ulipwe)

2. Kwa kutumia muda wako (Kuna watu wako bize na wewe una muda wa kutosha tu. Utumie kuwasaidia hao watu ili wakulipe)

3. Tumia ujuzi wako (Sasa sijui wewe una ujuzi gani, kama hauna ujuzi wowote futa app ya facebook kwa mwezi mzima Kisha ingiza app ya Coursera ukajifunze hata ujuzi mmoja huko).

4. Tumia akili yako kubuni kitu ambacho watu watakuwa tayari kulipia. (Unaweza kuandika kitabu, kuandaa ripoti, kutengeneza app na vitu vinginevyo)

5. Tumia kipaji chako

6. Tafuta ajira ili upate pa kuanzia.

7. Tafuta kitu chochote Cha kuuza, Kisha kiuze kwa bei ya juu kuliko ulivyokinunua

8. Uza vitu vyote ambavyo huvihitaji (simu, nguo za gharama, samani n.k)

9. Andika mpango mzuri wa biashara Kisha watafute watu walio tayari kuwekeza (hii itakuchukua muda sana na vile wabongo TUNAPENDA fedha ya haraka, wawekezaji wanaogopa wasije wakakupa fedha ukakimbia nazo, hivyo Jenga UAMNINIFU kwanza).

10. Tumia mtandao wa intaneti kuingiza fedha (mitandao ya kijamii, blogu au tovuti n.k)

11. Anzisha kijibiashara cha mtaji kidogo tu. Kisha kiendeleze.

Rafiki yangu usipate ujasiri wa kusema sina kitu cha kufanya. Kuwa bize kwa kufanya kitu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X