Kuna makosa matano ambayo watu wanafanya, kitu kinachosababisha watu hao warudi nyuma. Yaepuke makosa haya kama ukoma
Moja ni kosa la kununua bando la kuchati, kufuatilia maisha ya watu wengine.
USHAURI: KAMA hauna kitu cha maana cha kuongea na watu wala kufanya mtandaoni bora usinunue bando. Itumie hiyo fedha kuweka akiba au kuwekeza.
Pili, kuwekeza maeneo usiyoyajua
Hili ni kosa jingine. Watu wakisikia tu fursa fulani, wanakimbia kuwekeza kwenye hiyo fursa.
USHAURI: Ninachotaka ufahamu Ni kuwa si kila king’aacho ni dhahabu. Fursa nyingine unapaswa kuziacha zipite ili upate nguvu za kuwekeza maeneo machache unayoyajua. Pia, kabla ya kuwekeza sehemu hakikisha hiyo sehemu unaifahamu nje ndani. Tafuta taarifa zote unazoweza kupata kuhusu hiyo sehemu na zisome, Kisha chukua hatua sahihi
Tatu, kutomshirikisha mwenzi wako kwenye masuala yahusuyo fedha. Mwenzi wako wa ndoa anapaswa kujua mwenendo wa uchumi na mnapaswa kushirikishana mapato na matumizi yenu.
Mkue pamoja Kiuchumi, muwekeze pamoja na mkuze kipato chenu pamoja.
Nne, kununua au kuuza vitu unapokuwa na njaa
Hili ni kosa ambalo linaweza kukugharimu sana. Kwenye biblia kosa hili lilimgharimu kijana aitwaye Essau. Kijana huyu kwa sababu ya njaa tu alijikuta kauza haki ya kuwa mzawa wa kwanza.
Hii ikufundishe na wewe kuwa na wewe unapaswa kuachana na kufanya maamuzi hasa unapokuwa na njaa. Unaweza kukuta unauza nyumba ili upate buku ya kula kwa mama ntilie. Shauri yako.
Ukiwa na njaa utashangaa unaagiza chakula na vinywaji vingi, ila ukianza kula unakula kidogo tu, vingine unaviacha na pesa inapaswa kulipwa.
Tano, kununua vitu ili KUWARIDHISHA WENGINE. Hili ni kosa ambalo unapaswa kuliepuka.
Warren Buffet anasema kama unanunua vitu ili KUWARIDHISHA WENGINE, Kuna wakati utauza hata vitu ambavyo unavihitaji ili kupata fedha ya kula
Kumbe Mara zote nunua vitu vya muhimu tu, achana na vile ambavyo unaweza kuishi hata kama hujavinunua.
Ni hayo tu.
Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391