Mwandishi Anapaswa kutumia Muda Gani Kuandika Kitabu Na Kukikamilisha?


 Muda unategemea na topic unayoandikia.

Inategemea pia unaandika hiyo topic kama nani?

👉mtafiti

👉MBOBEVU

👉mtaalamu

👉mwanafunzi 

👉au unashirikisha UZOEFU wako.

Ila kwa vyovyote vile  kitu muhimu ambacho mwandishi yeyote yule atapaswa kufanya ni utafiti juu ya kile anachoandikia. Hii haijalishi wewe Ni mbobevu au una uzoefu mkubwa. Utapaswa kufanya utafiti juu ya mada yako. Na mara zote utakuta kuwa utafiti huo unakupa kitu kipya ambacho kitakuwa msaada kwako.

Wakati unaandika unapaswa kuwa na siku ya mwisho ambapo utakamikisha kitabu chako.

Mchakato wa uandishi wa kitabu una mambo mengi ndani yake kuanzia 

👉wewe kuandika draft ya kwanza.

👉kusoma draft yako na kuisoma tena na kuisoma tena (binafsi huwa napenda kusoma kazi yangu walau mara tatu) baada ya hapa

👉 kuna kuwapa watu wako wa karibu ili waisome kazi (hapa unachagua watu ambao au wanajua mada uliyoandikia au watu wanaopenda kusoma na ambao unakua wakisoma kazo yako watakupa mrejesho. Ni muhimu sana kufanya hivi maana hawa watu unaowapa kusoma kazi yako ni kama wawakilishi wa wasomaji wako. Hivyo, mrejesho wao unakupa picha ya namna wasomaji watakavyoipokea kazi yako. Pia hapa Ni MUHIMU SANA kuchagua watu waaminifu, la sivyo kazi yako wanaweza kuisambaza au hata kujimilikisha kazi uliyoifanya kwa juhudi kubwa.

Mwandishi tumia kipijdi hiki kupumzika kidogo na kufanya kama umesahau kazi yako. Ukiirudia tena kuisoma zamu ijayo utakuwa umeshapata kitu kingine chaa ziada.

👉 Baada ya hapo utairudia kazi yako wewe mwenyewe kwa kurekebisha yale waliyokushauri uyafanyie kazi wasomaji wako wa awali. Ni wazi pia na wewe utakuwa umepata mawazo ya ziada ya kuongezea au kupunguza ili kufanya kazi yako iwe bora.

👉kinachofuata Ni kumpa mhariri kazi yako 

👉 Kisha itafuata hatua ya uchapaji. Binafsi huwa nikituma kazi yangu kwa mhariri, muda huohuo naongea na mtu wa kutengeneza cover ya kitabu 

👉Mswada ukitoka kwa mhariri, kifuafacho ni wewe kufanyia kazi marekebisho aliyopendekeza mhariri Kisha kujiandaa kwa ajili ya kuchapa.

NB. 1. Siyo lazima upitie mchakto wote huo, ila kama umelenga kutoa kitabu bora unapaswa kuufuata. Binafsi huwa nafuata mchakato huu pale tu ninapokuwa ninatoa kitabu kwa mfumo wa nakala ngumu (hardcopy). Kwa soft copy vitu vingine huwa sivifanyii kazi.

2. Kama kuna watu ambao unajua watahusika kuandika chochote kwenye kitabu chako, mfano dibaji au neno (preview) unapaswa kuwapa taarifa mapema na kuwaomba wakufanyie hivyo. Ni muhimu pia ukiwashirikisha ratiba yako ya kutoa kitabu ili wakupe mrejesho mapema kama watakuwa na muda wa kusoma kitabu chako na kuandika unachotaka au la utafute wengine.

Ikumbukwe na hawa wapo bize na mambo yao. Hivyo kusema kwamba, utawapa kazi yako kirahisi waisome na kuifanyia kazi haraka ni nadra Sana.

Kwa msingi huo basi muda wa kukamilisha kitabu utategemea hivyo vitu. 

Kwa haraka inaweza kuwa hivi.

Kuandika draft (miezi mitatu)

Mwandishi kusoma draft yote mwanzo mpaka mwisho na kufanya marekebisho (mwezi mmoja)

Marafiki zako kusoma draft yako (mwezi mmoja). Hapa unaweza kuwapa walau marafiki watatu. Ila hakikisha ni waaminifu ili wasije wakasambaza kazi yako.

Kufanyia mrejesho wa marafiki zako (mwezi)

Mhariri (mwezi) 

Kutengeneza cover (mwezi. Binafsi huwa najipa muda wa kutosha kwenye kudesign cover. Hata yule ambaye huwa nampa kazi ta kutengeneza cover huwa namwambia mapema. Akitengeneza kava huwa ninakuwa na wiki moja au mbili ya kuitafakari. Kitabu ni kazi ya sanaa na kava ndiyo inaanza kuonesha hilo.

Kufanyia kazi marekebisho ya mhariri (wiki mbili)

Uchapaji (wiki mbili)

Sasa kwa msingi huo wewe unaweza kuanzia mwisho na kupangioia mtiririko wa matukio hayo, kisha kujua itakuchukua muda gani kukamilisha kitabu chako.

Nashauri usome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30: Kila Kitu Unachohitaji Kujua Kuhusu Uandishi Wa Vitabu Na Makala.

Hiki hapa

Kila la kheri.

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X