Nenda Viwango Vingine Wewe


Leo asubuhi nimeamka na kusikiliza wimbo wa William Yilima. Wimbo huu unaitwa Hii siyo ndoto yangu,

Naupenda wimbo huu maana mtunzi anataja baadhi ya vitu ambavyo siyo ndoto yake na hivyo ameamua na kuazimia kuwa hivyo vitu siyo ndoto yake. Badala yake ameamua kwenda viwango vingine

Mtunzi anaanza kwa kusema kwamba hii siyo ndoto yangu…

Hivi nilivyo siyo ndoto yangu, naaenda ng’ambo nyingine

Kuna mahali nimetoka na kuna mahali ninakwenda, hapa ninapita tu. hii siyo ndoto yangnu, naenda viwango vingine.

Ndani yangu naona nafasi nyingine

Mbele yangu naona viwango vya juu.

Ndani yangu naona kuinuliwa, naenda viwango vingine.

Mtunzi anaendelea kusema kuwa

Kuitwa mfanyabiahsara mdogomdogo, hii siyo ndoto yangu, ndoto yangu ni kumiliki biashara kubwa kimataifa.

Kuitwa muimbaji mdogo mdogo hii siyo ndoto yangu. ndoto yangu ni kuitwa muimbaji mkubwa kiulimwngu.

Kuitwa mfugaji mdogomdogo, hii siyo ndoto yangu. ndoto yangu ni kumiliki mifugo mingi isiyo na idadi, naaenda viwango vingine

Ndoto yangu ni kuwa mkulima mkubwa, naenda viwango vingine

Nimechoka kuitwa mchungaji mwenye kanisa dogo, naenda viwango vingine,

Kuna mahali nimetoka na mahali naenda. Hapa napita, naenda viwango vingine

Naenda viwango vya juu

Naenda viwanvo vya juu kielimu

Naenda viwango vya juu kiuchumi

Naenda viwanvo vya juu kihuduma….

 Mimi naishia hapo, ninachotaka kukwambia wewe leo ni kwamba na wewe unapaswa kuazimia kuhakikisha kwamba unaenda ngambo nyingine. Weka malengo makubwa na anza kuyafanyia kazi. hivyo ulivyo leo sivyo unavyopaswa kuwa kesho. Amua kwenda viwango vya juu. Wewe ni zaidi ya ulivyo leo.

Pia nakuomba utenge muda kidogo leo usikilize huu wimbo wa William Yilima. Ingia youtube andika Hii siyo ndoto yangu.

Nakutakia kila la kheri

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X