TATIZO LAKO WEWE


 

Kama naona jinsi utakavyoruka andiko hili . Maana umeona pameandikwa TATIZO LAKO, basi unaona ulipite ukaendelee na mambo mengine. Hutaki kujua tatizo lako ni nini.

Ndivyo ilivyo kwa wanadamu, mtu akisikia yanaongelewa matatizo ya wengine Basi ndio kwanza anatega sikio ili ayasikie vizuri wakati utakuta na mwenyewe  ana matatizo Kama hayohayo.

Tena unaweza kukuta ananyosha kidole kwa mwingine na kumlaumu kwa hali fulani wakati mwenyewe anafanya hivyohivyo kama yule anayemlaumu.

Looo!

Laiti hapa ningekuwa nimesema TATIZO LA DIAMOND, Nina uhakika wasomaji wangekuwa wengi.

Au ningesema TATIZO LA SAMIA. Basi WENGINE wangeitana ili kulichambua hili tatizo.

Na mimi nilivyo leo, sisemi tatizo la Mond wala Samia. Ni tatizo lako wewe.

1. Tatizo lako la kwanza hutaki kuambiwa ukweli. Kuwa mtu wa kupenda ukweli, na hata unapoambiwa ukweli kuwa TAYARI kuupokea na kuchukua hatua stahiki.

2. Tatizo lako la pili unapenda sana kufuatilia maisha ya watu wengine. Ngoja nikwambie, maisha ya wengine hayana manufaa Kama ya kwako. Fuatilia kwanza ya kwako. Usitake kunidanganya kuwa wewe unajali sana. Ndio maana unafuatilia maisha ya watu wengine. Weee! Jijali wewe kwanza.

3. Tatizo lako wewe unafanya Mambo yaleyale kila siku huku ukitegemea kupata mambo ya tofauti. Huo ni ujinga Kama alivyowahi kusema Albert Einstein.

4. Tatizo lako wewe, upo Tayari kuwekeza kwenye vitu visivyo na manufaa ila unasahau kuwekeza katika wewe. Unataka kwa nje uonekane vizuri wakati kwa ndani pameoza. Shauri yako wewe!

5. Tatizo lako wewe, umeendekeza uzembe kuliko kazi. Kijikazi kidogo tu eti umechoka. Asipokuwepo bosi, siku hiyo haufanyi kazi si ndio? NI mpaka usimamiwe ndio unafanya kazi.
Shauri yako wewe.

6. Tatizo lako malalamishi yamezidi. Kila wakati unalalamikia serikali, viongozi, wazazi n.k. Unahubiri mabadiliko lakini hutaki kubadilika. Kuwa mabadiliko unayotaka kuyaona wewe. Alishasema Mahatma Gandhi.

Niendelee au nisiendelee….

Nakupenda

Cheers!

Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391




One response to “TATIZO LAKO WEWE”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X