Maswali Manne Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Baada Ya Kusoma Kitabu


Kusikiliza Makala Hii BOFYA HAPA

Kwanza napenda ufahamu kuwa kila unapochukua kitabu basi walau unapaswa kupata kitu kimoja tu ambacho utafanyia kazi. Kama umesoma kitabu ukapata hata kimoja, inatosha; kifanyie kazi kwanza hicho kitu. Haifai usome kitabu halafu utoke bila kitu. Halafu kazi yako iwe kuwambia watu kuwa umeshasoma  kitabu fulani na kitabu fulani. Hilo sio lengo la kusoma vitabu.

Lengo ni kwamba ukisoma kitabu, upate kitu cha kufanyia kazi, na kweli ukifanyie kazi hicho ulichojifunza.

Sasa baada ya kuwa umepata kitu ambacho utafanyia kazi, unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo;

SWALI LA KWANZA; Nawezaje kutumia hiki nilichojifunza? Tafuta namna kitu ulichojifunza unavyoweza kukitumia kwenye maisha yako ya kawaida. Ukijiuliza swali hili, kaa chini uandike namna  ambavyo utaweza kukitumia.

SWALI LA PILI: Kwa nini nitumie hiki nilichojifunza?
Kuna ulazima wowote wa wewe kutumia hicho ulichojifunza. Ikumbukwe kuwa siyo kila kitu ulichosoma kinapaswa kutumiwa.

SWALI LA TATU: Wakati gani nitumie hili nilichojifunza?
Siyo mara zote unaweza kutumia kile ulichojifunza. Kwa mfano kanuni za mauzo Kuna sehemu yake ya kuzitumia  wakati ukijifunza kanuni za uandishi pia Kuna sehemu yake ya kuzitumia.
Hivyo jua sehemu sahihi ya kutumia kitu ulichojifunza.

SWALI LA NNE: Je, ninawezaje kufundisha hiki kitu kwa wengine?
Kama ulichojifunza kitakuwa na manufaa kwako basi kinaweza kuwa na manufaa kwa wengine pia. Hivyo, hicho kitu kizuri kisiishie kwako, tafuta namna ambavyo unaweza kukifundisha kwa wengine pia.

Hayo rafiki yangu ndiyo maswali manne ambayo unapaswa kujiuliza baada ya kuwa umesoma kitabu. Kisha yafanyie kazi.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


2 responses to “Maswali Manne Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Baada Ya Kusoma Kitabu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X