Siku ya leo, nimeona nikudokeze tabia muhimu ambayo unapaswa kuijenga kadiri unavyokuwa unaiendea siku yako. Na tabia hii siyo nyingine, bali ni tabia ya kufanya na kukamilisha majukumu yenye umuhimu mkubwa zaidi kwanza kabla ya kufanyia kazi majukumu mengineyo.
Ukianza kufanyia kazi majukumu yenye umuhimu mkubwa zaidi, hata luda wako ukiisha bila ya kufanya kazi nyingine, bado utakuwa umefaulu sana kuliko pale unapoanza na majukumu ambayo si ya muhimu kivile.
Kuanza na majukumu yasiyo na umuhimu kunakufanya uchoke huku ukiwa hujafanya kazi Kubwa au kitu chochote kikubwa.
Kwa hiyo, kitu cha KUZINGATIA siku ya leo ni kuwa unapoianza siku yako, hakikisha kuwa unafanyia kazi majukumu makubwa kwanza kabla ya kufanyia kazi majukumu mengineyo. Kila la kheri.
Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kujifunza namna ya kutengeneza fedha kupitia blogu tuwasiliane kwa 0755848391
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391