Vitu 10 ambavyo siyo lazima uwe kiongozi ili uvifanye


 

Umekuwa ni utaratibu wa watu wengi kuilalamikia serikali na kuitwisha mzigo kwa kila kitu hata kwa vitu ambavyo wao wenyewe wanahusika kuvifanya maishani mwao. Siyo kwamba naikingia mkono serikali ili usiiseme, ila ebu mwangalie mtu kama huyu hapa.

Kuna siku moja ambapo nilisikia jamaa analamlalamikia Magufuri kuwa ameshindwa kuiendesha nchi vizuri kwa sababu siku hizi hata watoto wake hawana adabu, wanavaa nguo fupi na hata wanavunja miiko mingi ambayo huko nyuma haikupaswa kuvunjwa na hasa kuvunjwa na watoto wenye umri kama huo.

Nilishangaa kidogo, yaani, mtu anamlalamikia rais kwa malezi mabovu ya wanae, unaona ee. Ni kama kituko fulani hivi. sasa siku ya leo ningependa tuongee, ndio ningependa tuongee mambo 10 ambayo siyo lazima uwe kiongoi kuyafanya. Bali unapaswa kuyafanya tu kwa ajili yako wewe mwenyewe;

1. kujali afya yako

Siyo lazima uwe kiongozi ili uweze kujali afya yako.. ni wazi kuwa afya yako ni kitu cha muhimu sana ambacho unapaswa kuthamini, ebu wewe mwenyewe ipe kipaumbele na ijali kwa viwango vikubwa bila kusukumwa na mtu yeyote yule. Ukiijali na kuitunza afya yako ni wazi kuwa unaenda kuwa na afya njema. Na afya njema ndiyo itakayokusaidia wewe kuweza kufanikisha malengo yako mengine ya kimaisha. Ukiwa na afya mbovu umelala kitandani muda wote, ni wazi kuwa hutaweza kufanya mambo mengine ya kimaendeleo, maana muda wote utakuwa ukihangaika na afya yako tu.

 

2. kuweka malengo

Hiki ni itu kingine ambacho siyo lazima uwe kiongozi ili ukifanye. Unapaswa kukifanya bila hata ya kusukumwa na mtu yeyote yule. Maisha yasiyo kuwa na melengo ni maisha ambayo hayafai. Ebu jiulize ni vitu gani ambavyo ungependa kupata na kufikia maishani mwako. Kisha amua kwa dhati kuviwekea vitu hivi malengo , na anza kuvifanyia kazi bila kuchelewa. usisubiri mpaka uambiwe weka malengo, ebu amua wewe mwenyewe kuwa sasa naweka malengo na ninayafanyia kazi kuanzia sasa.

 

3. Kujituma

Siyo lazima uwe kiongozi ili uweze kujituma kwenye kazi zako. kuna watu ambao mpaka awepo msimamizi nyuma yao ndiyo wanaaweza kufanya kazi ila asipokuwepo mtu kazi haifanyiki. Sasa napenda utambue kuwa siyo lazima uwe kiongozi ili uweze kujituma kwenye kazi ambayo wewe mweyewe unafanya. amua tu kuwa ninaaenda kujituma na ninaenda kufanya kazi kwa bidii kwa kila kitu ambacho nitaweka mkono wangu hata kama hakuna kiongozi yeyote yule nyuma yangu.

4. kusoma vitabu.

Usisubiri mpaka uambiwe na kiongozi kuwa soma vitabu. vitabu vipo kwa ajili ya manufaa yako, ili kukusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kufika mbali maishani. Kwa hiyo jenga utaratibu wa kusoma vitabu na kujifunza zaidi kutoka kwenye vitabu. ubora wa vitabu ni kuwa kwenye kitabu unakuta mtu amekushirikisha uzoefu wa kitu ambacho amekuwa akifanya kwa miaka 20 au 30 na kitu hicho anakiweka kwenye kitabu ambacho wewe unaweza kukisoma kwa wiki moja au mbili. Kiukweli hii ni kama kuiba hazina dhahabu. Utumie usomaji wa vitabu kama chanzo cha wewe kupata maarifa ambayo huwezi kuyapata sehemu nyinginezo. Ukishasoma maarifa haya, yafanyie kazi.

 

 

5.  kufanya vitu kwa utofauti.

Usisubiri uwe kiongozi ili uweze kufanya vitu kwa utofauti. Hapo hapo ulipo tafuta namna ambavyo unaweza kufanya kazi zako na shughuli zako kwa namna ya utofauti na vile ambavyo umezoea.

 

6. kuweka akiba

Umewahi kusikia mfuko wa hazina ee! Mfuko ambao serikali inaweka akiba yake, usisubiri mpaka kuje kuwa rais au waziri mkuu ili kuweka hazina serikalini, unaweza kuweka akiba yako hapo hapo ulipo kwa kipato hicho hicho ulichonacho. Halafu najua nini, akiba siyo lazima uweke fedha nyingi kwa wakati mmoja, badala yake ni kwamba unaweza kuanza kuweka fedha hata kama ni kidogo na kuendeleza kuweka fedha hiyo kila unapoipata, unajua nini? muda siyo mrefu utajikuta kwamba umeweza kuweka akiba kubwa ya fedha ambayo inaweza kukusaidia kufanya vitu vya maana kama kuanzisha biashara na kuwekeza.

 

7.kuanzisha biashara

Usisubiri mpaka uwe kiongozi ili uweze kuanzisha biashara, unaweza kuanzisha bishara hapo hapo ulipo kwa kutumia rasilimali hizo hizo ulizonazo au akiba uliyonayo. Tatizo lako unapowaza kuanzisha biashara basi unawaza kufanya kitu kikubwa ambacho kinahitaji mamilioni ya fedha, badala ya kuwaza hivyo, ebu waza biashara katika namna ambayo unaweza kuanza na kiwango kidogo cha fedha na hata kuendelea kuikuza mpaka kuifanya kuwa biashara kubwa. anzia hapo hapo ulipo kwa kufanya yale yanayowezekana na mwisho wa siku utajikuta kuwa unaweza kufanya yale yasiyowekezakana

 

8. kuwa mwaminifu

Moja ya tatizo kubwa sana la vijana wa kitanzania ni kupenda cha juu pale wanapokuwa sehemu ambayo wanapata fedha. Kitu hiki kimewafanya wengi wasiweze kuajirika na hivyo kukosa ajira hata kama zipo kwenye baadhi ya maeneo.  Kinachowafanya vijana wengi kukosa ajira ni kutokuwa waaminifu. Wengine wanaajiriwa na kufukuzwa kwa sababu siyo waaminifu. Sasa siku ya leo ninachotaka kukwambia ni kuwa unapaswa kuwa mwaminifu kwenye kazi zako na vitu vyote ambavyo wewe unafanya. iwe umeajiriwa au umeajiajiari. Hiki kitu kiomja tu  kinaweza kukupa fursa nyingiza kufanyia kazi, mpaka ukashangaaa.

 

9.kutumia kipaji chako

Najua, umezoea kuambiwa kuwa kipaji hakilipi bongo, ila tatizo wale wanaokuwambia kuwa kipaji hakilipi bongo hawajawahi kutumia kipaji chao wenyewe. Inawezekana wanachosema kina ukweli ndani yake, ila sasa kwa nini wewe uue kipaji chako kwa kisingizio eti hakililipi? Kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kutokana na kutumia kipaji chako. Na isitoshe kwenye ulimwengu wa leo ni rahisi sana kwako wewe kuwekeza kutumia kipaji chako na kutengeneza mazingira ya kipaji hicho kukulipa.

Najua utaanza kusema kwamba kazi nyingi za watu ambao huwa wanatumia vipaji vyao huwa zinaibiwa ila niachotaka ufahamu ni kuwa kwenye ulimwengu wa leo inawezekana kwa asilimia kubwa kutumia kazi zako katika namna ambayo hazitaaibiwa. Au labda tukubalinae kuwa kwa sasa kazi zinaibiwa. Lakini je, ikitokea kesho kikagunduliwa kitu cha kuzifunga kazi zikawa haziibiwi. Wewe utakuwa nayo hiyo kazi ya kufunga ili isiibiwe au ndio utabaki kusema kuwa sizitaki hizi mbich? Ebu badilika basi, anza kutumia kipaji chako, ujue ni kitu ulicho nacho ndani yako na unacho bure kabisa.

 

10. Kuea watoto wako

Mwanzoni tumeanza kwa kumwona jamaa aliyekuwa anamlalamikia Magufuri, kisa eti maadili ya watoto wake ni mabovu. Inashangaza ee! Ninachopenda kukwambia leo ni kuwa ni jukumu lako kuwalea wanao ili waweze uwa wenye manufaa kwa taifa la kesho.

 

Hivyo hapo ni vitu 10 ambavyo siyo lazima uwe kiongozi kuvifanya, unaweza kuvifanya hata kama ni mtu wa kawaida na vikawa vyenye manufaa makubwa kwako

 

Soma zaidi: Vitu Kumi Na Tatu Vya Kufanya Kipindi Hiki Ambapo Gharama Za Miamala Ya Simu Imepanda Bei

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X