Rafiki yangu, moja ya kitu ambacho watu wamekuwa wanakosea ni Kushindwa kuanza biashara huku wakisubiri wapate wazo bora la biashara.
Ninachopenda ufahamu ni kuwa wazo Bora la biashara halishuki kutoka mbinguni.
1. Wazo la biashara lipo kwenye huduma mbovu wanazotoa watu.
2. Unaweza kupata wazo bora la biashara kutokea kwenye matatizo yanayowakumba watu.
3. Unaweza kupata wazo bora kupitia kutembea.
Kumbe basi, wazo la biashara halishuki kutoka popote bali lipo hapohapo ulipo. Kitu kingine ni kuwa wazo bora la biashara haliwi bora kwa sababu umeliona. Wazo huwa linakuwa bora kupitia kulifanyia kazi. Ila wazo Kama wazo huwa siyo bora au baya.
Huwa mapenda kuwaambia watu kuwa wazo la kuanzisha Google halikuwa wazo bora. Ila hatua zilizochukuliwa baada ya kupata hilo wazo ndizo zililifanya liwe bora.
Hivyohivyo kwenye wazo la kuanzisha Facebook, twitter, Coca-Cola na kampuni nyinginezo.
Kwa msingi huo ndio kusema kuwa, ukitaka kulifanya wazo lako kuwa bora basi, lifanyie kazi.