Huu Ni Ugomvi ambao Unapaswa Kujiepusha Nao


 

Rafiki yangu, muda mwingine watu huwa tunajikuta tumeingia kwenye Ugomvi na watu. Tena kwa kujitakia kabisa. Leo nimeona nikwambie kitu komoja kinachofanya watu waingie kwenye ugomvi na jinsi ya kukiepuka. Kitu hiki ni kuwaonesha watu kuwa wanakosea. Ni wazi kuwa unaweza kuwa unaishi na watu ambao wanafanya vitu ndivyo sivyo.
1. Labda wanatumia fedha hovyo.
2. Wanajihusisha na michezo ya kubahatisha
3. Ulevi
4. Kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii.
5. Kuhonga n.k.

Sasa unaweza kuona ni bora uwasiadie kwa kuwaambia kuwa wanachofanya siyo sahihi. Hapo sasa  ndio unaweza kujikuta umejiingiza kwenye ugomvi usiokuwa wa lazima. Wataanza kukwambia fedha tunazitafuta wenyewe, hatutaki shida.
Wataanza kukwambia unawafuatilia maisha yao.

Ngoja nikwambie kitu, watu wengi huwa hawathamini ushauri ambao unawapa tena bure. Njia bora ya kuwasaidia hawa watu ni wewe kuhakikisha unakuwa bora kwenye kile unachofanya. Kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Kiasi kwamba wakuulize wewe umewezaje kufanikiwa hivyo. Kama ni kuwa na fedha, basi zitafute za kutosha sana kiasi kwamba waanze kukuuliza umewezaje kufikia viwango vya kuwa na fedha kiasi hicho.

Hapo sasa ndipo unaweza kuwahauri na kuwaonesha nini wanaweza kufanya.

Kwenye hili Mahatma Gandhi amewahi kusema kwamba unapaswa kuwa mabadiliko ambayo unapenda kuyaona. Hivyo, Kama Kuna mabadiliko ambayo ungependa kuyaona kwa watu wakiyafanya, anza kuyaonesha wewe kwanza.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X