Jinsi Habari Njema Zinavyoweza Kukufanya Upate Ushindi


 

Soma habari njema kwanza, kabla hujasoma habari mbaya

Tunaishi katika ulimwengu ambapo habari mbaya zinasambazwa kwa kasi kwelikweli kuliko habari njema. Hata hivyo kwenye ulimwengu huu unapaswa kuwa mtu wa kusoma habari njema zaidi ya unavyosoma habari mbaya.

Jiwekee utaratibu wa kusoma habari njema kwanza.
Ukiamka asubuhi, tafuta habari njema na uzisome.
Mchana, Soma habari njema na usiku soma habari njema.

Habari njema zinakutwa wapi?
Habari njema zinakutwa kwenye vitabu vya hamasa,  vya ujasiriamali, vya biashara na maendeleo binafsi, pia habari njema inaweza kukutwa kwenye kusikiliza vitabu vilivyosomwa, au vitu vingine vya aina hiyo.

Habari mbaya zimetapakaa mitandaoni, magazetini, redioni na maeneo mengine mengi.

Kuna umuhimu wowote wa wewe kupata habari njema?
Ndio, umuhimu upo. Habari njema zinakufanya uianze siku yako kwa namna chanya. Habari njema zinakufanya uendelee kuishi kwenye siku yako kwa namna chanya.
Habari njema zinakufanya ufikirie vitu vizuri vyenye manufaa kwako na kwa wengine pia.

Je, upo tayari kupata habari njema kwanza?

Ni imani yangu kuwa mpaka hapa, utakuwa umeamua kuwa sasa unaenda kujijengea utaratibu wa kupata habari njema kwanza, kabla ya habari mbaya m hivyo Anza leo kuchukua hatua.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X