Fursa Tano Ambazo Vijana Wa Siku Hizi Wanachezea (SEHEMU YA TATU)


Kama hukusoma sehemu ya pili bonyeza HAPA

3. Fursa ya kufanya kazi kwa bidii

Kwani kufanya kazi kwa bidii ni fursa? 

Na hapa ningependa nikurudishe tena nyuma mpaka miaka ya akina Napoleon Bonaparte. Umewahi kumsikia huyu mtu? Bonaparte alikuwa mbabe wa vita wa nyakati zake na pengine mbabe wa vita wa nyakati zote. Alipigana Sana vita na kushinda kwa kishindo kila mara. Ila moja ya kitu kilichokuwa kinamfanya Bonaparte kuwa wa tofauti, ni juhudi zake katika kazi. Alikuwa na juhudi kazini kuzidi juhudi zenyewe, hahaha.

Unaambiwa alikuwa anafanya kazi kiasi kwamba hata kama angekuwa bafuni, mtu akaja na nakala ya kusaini, alikuwa anatoka bafuni na sabuni mwilini, kusaini hiyo nakala Kisha anarudi bafuni kuendelea kuoga.

Siku hizi vijana ni kama tumepotea vile. Unakuta mtu anasafu mtandaoni asubuhi, mchana mpaka jioni, huku akiwa hazalishi chochote. 

Namkumbuka rafiki yangu aliyekuwa ananiambia eti mimi ninataka kazi ya kuwa naweka saini tu! Loo!

Hivi ni kweli yupo mtu ambaye kazi yake ni kuweka saini tu? Ebu kwa mfano tuseme yupo. Kama kweli yupo, Basi walau kuna vitu viwili ambavyo nitakuwa na uhakika navyo kuhusu yeye.

Kwanza ni mchapakazi. Anachapa kazi kwa viwango vya juu sana, kiasi kwamba ameaminiwa na kupewa kazi ya kusaini tu. 

Maana kazi ya kusaini tu inakuhitaji uwe mfuatiliaji ili kuhakikisha unachosaini kipo sawa. La sivyo unaweza kujikuta unasaini vitu visivyoeleweka ukapoteza kazi yako, cheo na kila kitu na hata kuwaharibia wengine.

Kazi ni gharama ambayo unapaswa kuilipa na kazi huwa haiangushi mtu.

Nimeandika kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA;  ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki ninaenda kukizindua rasmi tarehe 1.10.2021.

Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na kwa atayaweka oda;
Kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo.
Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.

Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa  vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.
Vitabu utatavyopewa kwa sasa ni
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA
3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.

Namba ya malipo ni

MPESA 0755848391
Airtel money: 0684 408 755
Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.

Karibu.

Vitabu vyote ni soft copy.

Ni mimi
GODIUS RWEYONGEZA
+255755848391
MOROGORO-TZ

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


One response to “Fursa Tano Ambazo Vijana Wa Siku Hizi Wanachezea (SEHEMU YA TATU)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X