Ngoja kwanza, kwani fursa ni nini? Unafanyaje ili kujua kuwa kitu fulani ni fursa na kingine siyo fursa. Kwani fursa huwa zinavaa vazi gani haswa?
Enewei, tuachane kwanza na maswali hayo japo nitayajibu mwishoni mwa makala haya, ila kwa sasa acha kwanza tuone fursa tano ambazo vijana wanachezea. Hizi fursa, japo zinachezewa sasa hivi, hazikuwahi kuwepo miaka nyuma, ila zimejitokeza kwenye zama hizi na bado zinachezewa. Mababu zako wangekuwa wanafufuka na kuona jinsi unavyochezea fursa hizi, wangeweza hata kukupiga viboko! Hahaha, natania tu!
Kwa kila fursa nitakueleza jinsi hali ilivyokuwa zamani, na jinsi hali ilivyo sasa hivi na mwisho kabisa, nitakueleza nini unaweza kufanya ili kuitumia fursa husika. Ngoja sasa tuanze.
1. Fursa ya kunoa kipaji chako na kukitangaza kwa gharama nafuu au bure kabisa
Ngoja turudi nyuma mpaka karne ya 15,16,17, 18…mpaka karne ya 20. Hapa tunakutana na wanasayansi maarufu wa nyakati hizo, akina Isaac Newton, akina Michael Faraday, akina Einstein na wengineo. Pia tunakutana na wagunduzi wa nyakati hizo; akina Henry Ford, Thomas Edison na wengineo. Bila kusahau waandishi,wachoraji na wasanii wote wa zama hizo. Hao niliowataja hapo walikuwa maarufu au walau walifanya kazi zilizogusa jamii ya kipindi hicho, na nyingine bado zina msaada mkubwa mpaka leo hii. Kazi za watu kama Picasso, Leonard Da Vinci, Shakespeare na wengineo.
Wakati hawa wanakuwa maarufu kwa gunduzi zao, maandishi ya ubunifu wao miaka hiyo, kuna wengine wengi walishindwa kutoboa kwa sababu ya kukosa namna ya kuwafikia watu sahihi ambao wangeweza kuwapa msaada wa kifedha kuwawezesha kunoa na kuinua vipaji vyao. Wengine walikosa nafasi kwenye majukwaa ili kuonesha kazi zao. Miaka hiyo kulikuwa na majarida na baadhi ya majarida, usingeweza kutoa chapisho lako kama wewe hukuwa mtu wa viwango fulani. Au kama hukuwa na konekisheni na mtu fulani.
Mfano mzuri ni Michael Faraday, huyu alizaliwa kwenye familia ya kimasikini, kipindi hicho Uingereza ilikuwa imewatenga watu kwenye kundi la wenye nacho (royal class) na wasiokuwa nacho (servant class). Na Faraday alikuwa kwenye kundi la pili. Kumbe hakuwa na ruksa ya kuchapa kwenye jarida kutokana na kundi alilokuwemo. Stori yake nitaieleza siku nyingine, ila fahamu kuwa jinsi alivyoweza kufikia viwango hivyo vikubwa mpaka kuwa mwanasansi mkubwa wa nyakati hizo, ilikuwa ni baraka kubwa sana kwake.
Kuna watu wengi enzi hizo walikuwa na vipaji hata kuwazidi wachoraji na wanasayansi wakubwa wa miaka hiyo. Ila hawakuweza kutoboa kwa sababu hawakuwa na konekisheni au fedha za kutosha.
Hiki kitu kwenye zama hizi kimepatiwa ufumbuzi kwa zaidi ya asilimia 80 Kama siyo 100 zote, hahaha.
Siku hizi ni rahisi sana kuanza kunoa kipaji chako hata kama huna konekisheni.
Kwa mfano ebu tuangalie miaka ya 1960. Kama wewe ungependa kuwa msanii na kutoa kazi yako, kulikuwa na mlolongo mrefu. Studio tu kurekodi wimbo wako ilikuwa mbinde. Na hapo hujaingia kwenye kuutangaza redioni, magazetini na kwenye runinga.
Ila sasa tuangalie kinyume chake. Siku hizi ni rahisi sana. Kwanza, ukiwa na kipaji cha kuimba tu, utatunga wimbo. Utaenda studio na kurekodi wimbo wako bila shida yotote ile. Baada ya hapo unaweza kuanza kuusambaza kwa ndugu zako, marafiki zako wa karibu na watu wengine unaoweza kuwafikia. Badala ya kuutambulisha wimbo wako redioni, unaweza kuutambulisha wimbo wako mtandaoni na watu wakausikiliza. Wakiupenda watawatumia wengine pia. Na hao wengine watawatumia wengine zaidi. Unaweza kujikuta kipaji chako kinakufanya uwe maarufu ndani ya muda mfupi sana.
Lakini je, ni vijana wangapi wanatumia hiyo fursa?
Ebu kwa mfano ona mambo yalivyokuwa kwa mwandishi. Kabla ya kuandika kitabu, ulipaswa kupata ruhusa kutoka kwa wachapaji wa vitabu iliyokuwa inasema, andika kitbu chako. Hapo ndio ulianza kuandika kitabu chako, kisha baada ya hapo, ulikipeleka kwa wachapishaji waliokupa ruhusa kukiandika ili wakisome. Kama wangekipenda, basi ulikuwa unapewa ruhusa ya kukichapa, ila kama hawakukipenda, uandishi wako ulikuwa unaishia hapo. Kipindi hicho kuna waandishi wengi kweli walishindwa kutoboa. Pengine hata babu yako alishindwa kuandika kitabu kwa sababu hiyo. Hahaha, hapo nimechomekea tu.
Ila sasa hivi mambo yamebadilika. Unaweza kuandika, kuchapa na kuuza kitabu chako ukiwa chumbani kwako. Unapata wazo na kuanza kuliandikia na baadaye unachapa na kuuza kitabu chako kwa njia ya mtandao. Unatengeneza fedha.
Siyo hivyo tu, nadhani siku za nyuma utakuwa ulisikia sana watu wanazungumzia bifu za wasanii na wamiliki wa vyombo habari na wasanii kutonufaika na kazi zao. Kama vyombo vya habari havikupenda kazi yako, basi
kiufupi hapo ulikuwa huwezi kusambaza kazi yako. Ila leo hii tunaye YouTube, habagui kazi za watu, wala hapendelei watu.
Tunayo majukwaa mengi ya kuonesha kazi zetu kama mtandao wa Amazon ambapo unaweza kuuza vitabu na bidhaa zako nyingine. Mtandao huu wenyewe haubagui bidhaa yako. Wewe kama unayo bidhaa yako unaweza kuuza, na ukiweza kutengeneza bidhaa nzuri, soko litakukubali na kuipokea kwa mikono miwili. Kitu hiki babu yako asingeweza kukifanya miaka ya 1920.
Kumbe zama zimebadilika. Maisha yamebadilika na mtandao wa intaneti unaleta fursa nyingi kweli kwelikweli. Kazi ni kwako kuzitumia.
Kwa leo naishia hapa, ili nikuachie nafasi ya kutafakari ulichojifunza mpaka hapa. Kesho tutaendelea na fursa namba 2 inayochezewa na vijana kwenye zama hizi.
Ila kuna kitu kimoja nimekumbuka, mwanzoni mwa makala hii, nilianza kwa kukuuliza, kwani fursa ni nini?
Unafanyaje ili kujua kuwa kitu fulani ni fursa na kingine siyo fursa. Kwani fursa huwa zinavaa vazi gani haswa?
Kujibu maswali hayo na mengine, nimeandika kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki ninaenda kukizindua rasmi tarehe 1.10.2021.
Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na kwa atayaweka oda;
Kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo.
Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.
Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.
Vitabu utatavyopewa kwa sasa ni
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA
3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.
Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.
Namba ya malipo ni
MPESA 0755848391
Airtel money: 0684 408 755
Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.
Endelea na SEHEMU YA PILI KWA KUBONYEZA HAPA
Karibu.
Vitabu vyote ni soft copy.
Ni mimi
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
MOROGORO-TZ