Mambo 100 Ya Kujifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Rich Dad Poor Dad


Kitabu: RICH DAD POOR DAD
Mwandishi: Robert Kiyosaki
Mchambuzi: Hillary Mrosso
Simu: +255 683 862 481

UTANGULIZI

RICH DAD POOR DAD, ni kitabu cha ajabu sana, tangu kiandikwe zaidi ya miaka 25 iliyopita kimeleta mageuzi makubwa sana kwenye maisha ya watu, makampuni, biashara, fedha, uwekezaji, uongozi, ujasiriamali na utajiri. Ni kitabu ambacho kinaelezea mifumo ya maisha na vipaumbele vya wazazi wawili ambao mmoja ni tajiri na mwingine ni masikini. Kila mmoja alikuwa na mitazamo yake yanapokuja masuala ya kifedha, utajiri, uwekezaji, biashara, elimu na hata malezi ya watoto. Katika uchambuzi wa kitabu hiki nitaelezea kwa kina mambo haya. Ninaweza kuungana na watu wengine mashughuri waliosema hiki ndio moja ya kitabu bora sana kuwahi kuandikwa katika karne hii kuhusu masuala yote muhimu ya kifedha uwekezaji. Nakukaribuisha katika uchambuzi wa kitabu hiki tujifunze kwa kina mambo 100 niliyoyaona katika kitabu hiki cha RICH DAD POOR DAD.

1. Kati ya vitu alivyosisitiza sana mwandishi wa kitabu hiki ni jinsi elimu ya fedha ilivyo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku. Mwandishi ametilia sana mkazo katika kupata maarifa sahihi ya fedha yatakayotutoa kwenye umasikini wa kipato na kutufanya kuwa matajiri.

2. Mfumo wetu wa elimu ulivyoshindwa kutuandaa katika maisha halisi ya duniani yanayohusu fedha na uwekezaji. Badala yake mfumo umejikita kutuandaa kuwa wataalamu wa kuifanyia pesa kazi ili tupate utajiri.

3. Mfumo wetu wa elimu hautoi elimu ya msingi ya kupata fedha, kutengeneza fedha, kutunza fedha na kuzalisha fedha.

4. Hata familia zetu zimejikuta zikiishi mfumo huo wa elimu na kukosa kabisa somo la fedha, na wazazi wetu hawajui hilo, ndio maana wanawekeza nguvu sana kwenye kupata elimu ya chuo pekee.

5. Tunatakiwa kubadilika haraka na kuacha kufikiri elimu ya chuo pekee ndio itatutoa kwenye umasikini.

6. Elimu ya chuo tunayoipata ina mapungufu mengi hasa kwenye kipengele cha fedha, haituandai jinsi ya kutatua changamoto za kifedha.

7. Nadharia ya kusoma kwa bidi, upate maksi kubwa, ili uje kupata kazi nzuri na salama inayolipa, inaweza kuwa sio ushauri mzuri sana kwa zama hizi.

8. Kama unataka kuwa tajiri, jua kuwa unahitaji sana kuielewa fedha kiundani nasio kujua kufanya kazi kwa bidii pekee.

9. Ni ngumu sana na hutaweza kuwa tajiri kwa kutegemea ajira pekee, jifunze namna ya kuzalisha fedha jitaidi kuwekeza kwenye vitu vinavyokuingizia fedha.

10. Kazi kubwa ya kufanya kama unataka kufikia utajiri na kuwa na uhuru wa kifedha ni kujielimisha kila wakati kuhusu mambo ya kifedha.

11. Mengi tunayojifunza ni namna ya kutumia pesa kwenye mambo yasiyozalisha fedha, na hapo ndio changamoto kubwa huanzia. Mfano kununua vitu vingi visivyokuingizia fedha.

12. Mwandishi ameonyesha sehemu kubwa ya maisha yetu tunajua kutumia tu vifedha kidogo tunavyopata, na huvitumia katika kununua vitu visivyozalisha (liability) badala ya kununua vitu vinavyozalisha fedha (asset).

13. Mwandishi anashauri sana tutafute progamu na mafunzo ya kutuelimisha kuhusu fedha, ni somo muhimu sana kwenye zama hizi.

14. Mwandishi anapendelea kila mtu kujua kuhusu uhasibu na uwekezaji maana huko ndio msingi wa fedha na usimamizi wake huanzia.

15. Tunashauriwa kujitoa kwenye mbio za panya, ambazo ni mzunguko wa maisha unaojirudia rudia na hauna tija wala machango katika safari ya kukufanya kuwa tajiri na kuwa huru kifedha.

16. Tunatakiwa kubadili mbinu katika mchezo, maana hatuwezi tena kuendelea na mbinu za zamani ambazo haziwezi kutatua changamoto za kifedha tulizonazo.

17. Kumbuka mitaala mingi ya elimu imeandaliwa kutufanya wafanyakazi, wanaoifanyia kazi pesa, kwa malipo kidogo.

18. Pia kupitia uzoefu wake akiwa nyumbani anasema somo la fedha ni gumu zaidi kufundishwa nyumbani kuliko vyuoni. Hii ni kutokana na mfumo wa elimu na namna watu na wazazi wetu walivyoaminishwa kuhusu fedha.

19. Wazazi wengine huwaambia watoto wao kuwa fedha sio nzuri, na watu wanaopenda fedha wana roho mbaya, ni watu wenye tamaa na wasiojali wenzao. Mambo kama haya mtoto anakuwa akijua fedha sio nzuri na hana haja ya kuipa kipaumbele kama sehemu muhumu ya maisha.

20. Tofauti na matajiri, wao hufundisha watoto wao misingi ya kupata fedha, kutunza fedha, kuzalisha fedha na huwafundisha watoto wao namna ya kutoa fedha na kuwasaidia wengine.

21. Ujinga mwingi tulio nao kwenye mambo ya fedha ndio hutuletea changamoto za kifedha za kila siku.

22. Tunatakiwa kuziruhusu akili zetu zifanye kazi inapokuja suala la fedha, na sio kuzizuia kama wengi wanavyofanya, ipe akili yako majukumu ili ihangaike kukutafutia suluhisho la changamoto za kifedha.

23. Husisha na tumia akili zaidi linapokuja suala nyeti kama la fedha, tumia akili zaidi kuliko hisia. Hii ndio njia ya kulinda matumizi mabaya kwenye fedha zako.

24. Ruhusu changamoto za maisha zishughulishe akili zako ili kukupatia suluhisho kwenye changamoto za kifedha unazokutana nazo.

25. Kamwe usikubali wala kuruhusu changamoto za maisha zikufanye ushindwe na kuwa mnyonge au zikuharibu, zitumie kwa faida yako maana ndio mwalimu mzuri.

26. Utajua una uwezo mkubwa kiakili pale unapoipa akili yako majukumu ya kufikiri kila wakati, usizimishe uwezo huo ambao umepewa na Mungu, kila mtu ana uwezo huo, uache utokee na ukusaidie kifedha.

27. Jitahidi sana kutokuogopa, ondoa hofu zinazokupeleka kwenye umasikini wa kipato, dhibiti kabisa na uwe tayari kuchukua hatua za kijasiri ili utoke kwenye umasikini.

28. Inahitaji ujasiri na moyo mkuu kuamua kutoka kwenye mazoa na tabia zinazokurudisha nyuma kifedha, amua kwa dhati inapofikia unataka kubadilika na kuwa tajiri, sio safari nyepesi.

29. Usiruhusu hofu ikutawale maana utashindwa kuchukua hatua za kijasiri kujitoa kwenye umasikini na madeni, hofu inakufanya unakuwa mtumwa wa fedha.

30. Kumbuka siku zote serikali huwa ndio ya kwanza kuchukua fedha zako kama kodi, na watakata kodi unapopata fedha zako, watakata kodi unapozitumia, watakata kodi unapozihifadhi, wanakata kodi hata utakapokufa.

31. Wanaolipa kodi nyingi ni watu masikini na watu wa kati walioajiriwa, matajiri hawateseki na kodi kama masikini.

32. Waajiriwa wengi wanawalaumu sana mabosi wao kwa matatizo waliyonayo wao wenyewe.

33. Mfumo wa maisha ya wengi ni kama vile wamezaliwa kuja kufanyia kazi watu wengine na kisha wakipata fedha wakalipe kodi wanazodaiwa.

34. Pesa ina nguvu sana, jitahidi kutumia hiyo nguvu kukufanikisha kwenye maisha na sio hiyo ngumu iwe kinyume chako.

35. Dhibiti kabisa hisia na tamaa zako linapkuja swala la fedha maana usipofanya hivyo utaishi kwa hofu na kamwe hutaweza kuwa tajiri.

36. Kwa kiasi kikubwa umasikini na changamoto nyingi hunasababishwa na ujinga kwenye masuala ya kifedha.

37. Hakuna kuhitimu chochote kwenye maisha, usihitimishe elimu yako, jifunze kila siku hata kama umefikia hatua kubwa kwenye maisha.

38. Wengine wakimaliza chuo ndio basi tena hakuna cha kujifunza tena, na hapo ndio kiburi huzaliwa na kuwazuia wasijifunze chochote maana huona wanajua kila kitu.

39. Tumia hisia zako kufikiri na sio kufikiri kwa kutumia hisia hasa kwenye mambo ya fedha.

40. Mara nyingi sio kazi rahisi kuwapata wafanyakazi au wasimamizi waaminifu na wazuiri, ni kazi sana kuwapata, jua hilo siku zote.

41. Pesa bila kuwa na akili ni sawa na kupoteza tu.

42. Muhimu kwenye fedha sio kujua tarakimu tu, bali kujua maana na hizo tarakimu zinaashiria kitu gani.

43. Ni muhumu kuelewa ujumbe ambao unaupata hasa kwenye masula ya fedha na uwekezaji, elewa maana ya ujumbe huo kwa kina.

44. Jifunze kusoma taarifa za kifedha na kuzielewa, ili uboreshe biashara yako.

45. Pambana uwezavyo kuondoa kabisa ujinga hasa kwenye masula ya fedha, pata kila elimu kuhusu fedha jinsi inavyofanya kazi na jinsi inavyoweza kukufanyia kazi.

46. Elewa kwa undani kuhusu asset na liability, kamwe usichanganye, maana ndio zitaamua uhuru wako wa fedha kwa siku zijazo.

47. Asset ni vitu ambavyo vinakuingizia fedha, au vitu ambavyo vinaweka fedha mfukoni mwako.

48. Liability ni vitu ambavyo hutoa fedha mifukoni mwako, yani vitu ambavyo havikuingizii fedha.

49. Kama unataka kuwa tajiri mapema zinagatia sana katika kuwekeza kwenye asset na sio liability.

50. Kama huna matumizi mazuri ya fedha, hata ukiongezewa fedha nyingi pia hutakuwa na matumizi mazuri, zaidi utazidisha matumizi mabaya ya fadha zako.

51. Changamoto nyingi za kifedha tunazopitia ni kutokana na kufuata mkumbo na kununua vitu ili kuwafurahisha wengine.

52. Watu wenye akili huajiri na hufanya kazi na watu wenye akili zaidi ili wazidi kufaninkiwa
53. Ukizidisha hisia sana inaweza kuathiri hata uwezo wako wa kifedha unashuka.

54. Moja ya maana ya utajiri ni kuwa na uwezo wa kuishi siku nyingi zaidi bila kufanya kazi yoyote na kuweza kumudu gharama zote za maisha.

55. Utajiri unapimwa kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha kwenye asset zako.

56. Matajiri mara azote hununua asset au vitu vitakavyowaingizia fedha zaidi, masikini na watu wa kati wenyewe hupenda matumizi na kununua vitu visivyowaingizia fedha.

57. Matajiri wataendelea kuwa matajiri na masikini watendelea kuwa masikini kwasababu wanatofautiana sana katika matumizi yao ya fedha.

58. Changamoto nyingi za kifedha huwa zinatokana na watu kutumia muda mwingi wa maisha yao kuwafanyia wengine kazi, au kuajiriwa au kukaa katika ajira.

59. Hatari au risk inapungua pale unapopenda kuwekeza na kuelewa uwekezaji kwa ujumla, uelewa hupunguza hatari.

60. Kila fedha inayongia kwenye uwekezaji wako, ifanye ikufanyie kazi kama mtumwa wako.

61. Tumia uwezo wako wa kiakili kifedha ili kupata vitu unavyovitamani katika maisha yako.

62. Kama unaifanyia kazi fedha, pesa itakutesa, pesa itakunyanyasa, na siku zote hutakuwa na sauti kwa mwajiri wako. Pesa inatakiwa ikufanyie wewe kazi.

63. Jitahidi kutengeneza sauti yako, kwa kuwekeza na kujizoeza kujifunza masula ya kifedha kwa undani ili uimiliki fedha, na sio fedha ndio ikupelekeshe.

64. Pambana kutafuta uhuru wako kifedha, jitie bidii kujitoa kwenye umasikini kwa kujifuza kuhusu fedha.

65. Moja ya sifa kuu za kitajiri ni kuwa na uweza wa kusoma taarifa za kifedha na kuzielewa barabara.

66. Misingi mikuu ya kuwa na uwezo wa kiakili kifedha ni kuelewa mahesabu ya fedha (accounting), uwekezaji, masoko na masuala ya kisheria.

67. Ni muhimu kuwa na shirika au kampuni yako katika safari za kusaka utajiri.

68. Kwenye safari ya kuwa tajiri na kufikia uhuru wa kifedha wengi wanarudishwa nyuma na hofu zao wenyewe, kutokujiamini.

69. Hofu na kutojiamini kunaondoa na kudumaza uwezo wako wa akili kwenye mambo ya fedha.

70. Safari ya kuwa tajiri inahitaji akili na ujasiri mkubwa maana changamoto ni nyingi.

71. Watu wengi linapokuja suala la hela wanachojua na ujuzi walionao ni kufanya kazi kwa bidii tu.

72. Tunashauriwa tusifanyekazi tu kwasababu tunalipwa,bali tufanye kwasababu tutanajifunza.

73. Ifanye pesa iwe mtumwa wako, pesa ikufanyie kazi na sio vinginevyo.

74. Muhimu kuwa na ujuzi katika haya; Usimamizi wa mzunguko wa fedha, usimamizi wa mifumo muhimu kama familia, muda, usimamizi wa watu.

75. Watu wengi walio bize ni wavivu kufuatilia masula muhimu kama masuala ya fedha.

76. Wengi wanatumia kiburi kuficha ujinga wao maana hawapo tayari kujifunza.

77. Kila kipato unachopata kwenye maisha yako, jilipe mwenyewe kwanza.

78. Tengeneza nidhamu ya juu sana kuhakikisha kila kipato unachpata unajilipa mwenyewe kwanza, kisha ndio ulipe mambo mengine kama vile kodi.

79. Tumia pressure ya wanaokudai kutengeneza njia nyingine za kukuinginzia kipato ili uweze kuwalipa.

80. Kuwa mtoaji, unapofanikiwa kifedha na unapopungukiwa kifedha jambo muhimu la kufanya ni kuwa mtoaji.

81. Walipe vizuri wafanyakazi wako, maana hao ndio wanakusaidia mambo mengi kwenye biashara yako.

82. Elewa kuwa asset ndio hununua vitu vya anasa au luxuries.

83. Kopa pesa ili uzalishe pesa na sio vinginevyo.

84. Kuwa na mtu unayemwangalia kama model au shujaa wako kwenye safari yako ya utajiri, angalia waliofanikiwa na wanaofanya unachotaka kufanya.

85. Wafundishe wengine mambo unayoyajua kuhusu maisha na fedha, kwa kufanya hivyo utapokea mara nyingi zaidi ya kile ulichotoa.

86. Ni vizuri sana kama hutoingia au kuwa na madeni kwenye maisha yako.

87. Kanuni ya maisha kama unataka chochote, basi jufunze kutoa kwanza na sio tofauti na
hapo.

88. Kama kuna kitu chochote unakitaka kwenye maisha, toa kwanza kile ulicho nacho, ndio utapata unachokitaka.

89. Masikini wengi ni wachoyo na wana roho mbaya, wanasubiri wafanyiwe kitu kwanza ndio na wao wafanye, yani wapokee kwanza ndio nao wawe watoaji.

90. Acha kufanya unachofanya, chunguza na pitia maisha yako kwanza angalia vinavyofanya kazi na vinavyokupotezea muda.

91. Chukua Jukumu la kushughulikia masuala yako ya kifedha, usimuachie mtu mwingine.

92. Jifunze sayansi ya kutengeneza fedha.

93. Tafuta mawazo tofauti, katika uwekezaji, kisha chukua hatua mara moja.

94. Tafuta aliyefanya uanachofanya.

95. Tafuta mafunzo na madarasa ya kujifunza, nunua mafundisho.

96. Tangeneza offa.

97. Tembea maeneo tofauti ujifunze.

98. Angalia sehemu sahihi

99. Chukua hatua

100. Anza mapema uwezavyo.


3 responses to “Mambo 100 Ya Kujifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Rich Dad Poor Dad”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X