Watalaam wa Biblia wanasema kwamba kwenye Biblia kuna usiogope 365. Maana yake kila siku ukiamka unaambiwa usiogope.
Usiogope maana uoga wako ndio utakufanya uendelee kuishi maisha yaleyale kila siku bila kufanya kitu Cha tofauti ambacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa maishani mwako. Usiogope maana uoga wako ndio umasikini wako. Ukiogopa, hutachukua hatua yotote, kitu ambacho kitakufanya ushindwe hata kufanya vitu ambavyo vingekuletea maendeleo.
Ukiendelea kuogopa na kufikiri kuwa watu watanionaje. Utashindwa kufanya kitu chochote cha maana.
Unapaswa kuipiga chini, misuli ya uoga ili uweze kufanya vitu vinavyoeleweka.
Neno uoga kwa kiingereza linaitwa FEAR. Kirefu chake ni False Evidence Appearing Real.
Hii ndio kusema kuwa vitu vingi unavyoviogopa siyo sahihi na asilimia kubwa havitakuja kukutokea kama unavyodhani. Na vitakavyokutokea havitakuwa na madhara kama unavyodhani.
Uoga una madhara mengi sana, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukuua. Hivyo, achana na uoga vaa vazi la ujasiri.
Muda ambao utaanza kujiambia kuwa ngoja niache, nisifanye kitu fulani kwa uoga. Amua ukifanye. Utanufaika zaidi kwa kukifanya hicho kitu kuliko kuendelea kuogopa.
Kila la kheri.
Soma zaidi: Ijue maana nzuri ya MASIKINI
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri