Vitu Vitano Ambavyo Havitabadilika Miaka Kumi Ijayo


 

Vimeandikwa vitabu vingi sana kuhusu mabadiliko. Vinaeleza kuwa unapaswa kubadilika maana mambo yanabadilika. Mimi pia nimekuwa nikiandika kuhusu mabadiliko ila leo ninataka kukwambia vitu vitano ambavyo havitabadilika miaka 10 ijayo.

Ubora ni kuwa ukivijua vitu ambavyo havitabadilika, unaweza kuvitumia kwa manufaa na kuvifanya kuwa fursa. Hivyo, hivi hapa ndivyo vitu ambavyo havitabadilika ndani ya miaka 10 ijayo;

1. Watu kupenda vitu vizuri kwa bei rahisi

Hiki ni kitu ambacho kitaendelea kuwa kipaumbele kwa watu. Watu wataendelea kupendelea kupata vitu vizuri kwa tena kwa bei rahisi sana. Na hii ishara kuwa hii inaweza kuwa fursa nzuri kwako. Ni fursa kwako kuanzisha biashara katika msingi ambao utakuwa ukiwasaidia watu kupata huduma nzuri, tena kwa bei nafuu.

2. Watu wataendelea kupenda kupata huduma kwa haraka

Sasa hivi tupo katika kipindi ambapo watu wanapenda kupata huduma nyingi kwa haraka kweli. Ndio maana siku hizi utasikia kuna magari ya mwendokasi, mitandao ya simu inajinadi kwa intaneti  yenye kasi, kuna migahawa inayotoa chakula cha haraka (fast food), hii yote ni kuonesha kuwa vitu vya haraka vinahitajika sasa hivi na vitaendelea kuhitajika kwa siku nyingi zijazo. Huduma  za kutuma fedha kwa haraka kama mpesa na tigo pesa zimekuwa maarufu, kwa sababu zinatoa nafasi ya kupata huduma ya kifedha kwa usalama, uhakika na haraka.

Hii nayo ni fursa unayopaswa kuangalia namna ya kuitumia.

3. Kula chakula

Ndio, watu wataendelea kula na kunywa ndani ya miaka 10 ijayo. Hawataacha kula wala kunywa. Hii nayo ni fursa ambayo unaweza kuitumia kwa manufaa yako. Unaweza kwa mfano kuanzisha mgahawa kwa ajili ya kuwapatia watu chakula, unaweza kuongeza thamani ya vyakula, unaweza kuingia sahambani kulima, unaweza kuwa msambazaji wa chakula n.k. hapa napo fursa ni nyingi.

4. Saa 24 kwa siku

Sidhani kama kitagunduliwa kifaa cha kuongeza muda ndani ya miaka kumi ijayo. Hivyo, muda utabaki kuwa saa 24 kwa siku. Hii nayo ni fursa, japo saa zitabaki kuwa 24 ndani ya muda huu ila majukumu  ya watu yataongezeka na wewe unaweza kuwa mtu utakayewasaidia hawa watu kwa kurahisisha au hata kufanya majukumu yao yaliyoongezeka. 

Angalia kitu ambacho unachoweza kurahisisha na jikite hapo.

5. Watu wataendelea kupenda kupata uhakika wa huduma wanazopata. Watu watahitaji uhakika. Uhakika kuwa wanatumia fedha zao sehemu sahihi, uhakika kuwa wewe ni mtu sahihi, uhakika kuwa bidhaa zako ni bora kuliko nyingine, n.k.

Na wewe unapaswa kuwapa uhakika watu hao. Ndio maana siku hizi, utaona watu wanatoa bidhaa na guarantee. Hii yote ni kwa ajili ya kuwapatia uhakika wateja.

Kwa Leo naishia hapo.

Hayo ndiyo mambo matano ambayo hayatabadilika ndani ya miaka 10 ijayo. Hivyo, kama upo makini,  unaweza kuchagua eneo moja na kuligeuza kuwa fursa ambayo wewe utachangamkia.

Nimeandika kitabu, kinaitwa MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki kimezungumzia sana juu ya suala zima la fursa, jinsi ya kuziona na kuzitumia kwenye maisha. Na kitabu hiki kitazinduliwa rasmi tarehe 1.10.2021.

Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na atayaweka oda; kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo. Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.

Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa  vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu Cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.

Vitabu utkavyopewa kwa sasa ni 

1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA

3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.

Namba ya malipo ni 

MPESA 0755848391

Airtel money: 0684 408 755

 Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.

Karibu.

Vitabu vyote ni soft copy.

Ni mimi

GODIUS RWEYONGEZA

0755848391

MOROGORO-TZ


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X