ZEGE HALILALI


Wajenzi wanalifahamu hili. Zege ikichanganywa, kwa vyovyote vile hata iweje, inapaswa kuisha, la sivyo ikilala, asubuhi, hutaikuta kama zege, badala yake itakuwa imekauka.

Itakuwa siyo zege tena…
Itakuwa haifai tena kwa ajili ya ujenzi.
Ndio maana huwa wanaenda kwa kanuni ya zege HALILALI.

Na wewe unaweza kujiwekea utaratibu kama huu. Kuna vitu katika maisha yako unapaswa kuvifanya kuwa kama zege. Na havipaswi kulala hata kidogo. Vifanye siku hiyohiyo na uvikamilishe.
Kama kuna majukumu ya kuandika, hata kama ni maneno kidogo, hakikisha unayaandika kila siku bila kulaza kiporo. Maana zege halilali.
Kama unapaswa kufanya mazoezi yafanye maana zege HALILALI.
Kama unapaswa kuweka akiba leo, usiseme kwa kuwa kesho nitapokea fedha nyingine ngoja ya leo niitumie nitakuja kuweka akiba ya kesho au kesho kutwa. Kumbuka fedha ya leo inapaswa kuwekewa akiba yake na kesho inapaswa kuwekewa akiba yake pia.

Kwako fanya vitu kama hivyo kuwa mwiko. Vifanye kuwa kama zege, maana ZEGE HALIPASWI KULALA.

Ni kitu gani unaenda kukifanya kuwa kama zege leo?
*******************************************************

Nimeandika kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA;  ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki ninaenda kukizindua rasmi tarehe 1.10.2021.

Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na kwa atayaweka oda;
Kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo.
Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.

Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa  vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.
Vitabu utatavyopewa kwa sasa ni
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA
3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.

Namba ya malipo ni

MPESA 0755848391
Airtel money: 0684 408 755
Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.

Karibu.
Godius Rweyongeza
+255755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X