Kwenye kitabu hiki Erick Shigongo ameeleza historia ya maisha yake na kutoa mafunzo kadha kadha kuhusu maisha
Kitabu hiki ni kizuri sana, nashauri kila mwenye kiu ya mafanikio makubwa akisome. Utajifunza mengi kuhusu kutoka umasikini mpaka mafanikio makubwa kupitia stori ya Erick Shigongo ambaye maisha yake yalikuwa duni sana, kuliko hata wewe ila akaweza kupasua anga na kufikia viwango vikubwa.
Utajifunza na kuona ni kwa jinsi gani na wewe unaweza kufanikiwa pia kupitia mbinu mbalimbali alizoshirikisha mwandishi huyu.
Moja ya kitu ambacho nakikumbuka sana kutoka kwenye kitabu hiki ni kauli inayosema kwamba; Kuna watu kwa tabia zao wataendelea kuwa masikini na Kuna watu kwa tabia zao hata waukimbie utajiri, utazidi kuwafuata tu.
Leo nimeona nikushirikishe hili ili na wewe ujitathimini tabia zako. Hivi ni kweli wewe ukiamua kuukimbilia utajiri utakufuata kweli au utaendelea kuwa masikini tu kutokana na tabia zako?
Jiulize una tabia gani. Na je, hizo tabia zinakupeleka wapi?
Soma zaidi:
Watanzania Tujenge Utaratibu Wa Kukubali Vitu Vyetu.
Kila la kheri.
GODIUS RWEYONGEZA
Morogoro-Tz