Madhara Ya Kuwa Na Mahusiano Na Mtu Zaidi Ya Mmoja


 

Kama una ndoto kubwa na umekuwa na mpango wa kuja kuwa na mahusiano na watu wawili, au tayari una mahusiano na watu wawili ni bora ukauhairisha au kuondoa kabisa huo mpango. Yafuatayo ni mdhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja.

Kwanza utapoteza nguvu zako nyingi kwa watu hao ambao umeingia nao kwenye mahusiano. Hizi ni nguvu ambazo ungeweza kuzitumia kufanya kazi zako za maendeleo.

Pili, utapoteza muda wako ambao ungeweza kuutumia kufanikisha NDOTO zako.

Tatu, utapoteza fedha ambazo zingekusaidia kufanikisha NDOTO zako kubwa. Na kama unavyojua muda ni mali.

Hayo ni madhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja. Epuka kitendo hiki kwa nguvu zako zote.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X