Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!


 

Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene.

Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha.

Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki wanasisitiza ni kutoogopa.

50 Cent anasema kitu kikubwa ambacho unaweza kukiambatanisha na maisha yake ni kutoogopa. Yeye haogopi chochote kile maishani mwake. Na hicho kitu ndicho kimemfanya ashinde vikwazo ambavyo huwa hata vinawazuia watu kuchukua hatua ya kwanza.

Waandishi wanasisitiz kwamba, usiogope. Kamwe usiogope kabisaaa kwenye maisha yako.

Na mimi Leo napenda kukusisitiza kwamba usiogope 

Kama wewe huwa unasoma Biblia, watalaamu wanakwambia kwamba kwenye Biblia Kuna USIOGOPE 365. Hivyo, hata Leo ulipoamka asubuhi, umeambiwa usiogope.

USIOGOPE


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X